title : MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU
kiungo : MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU
MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU
Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeupa muda wa siku tano kuwasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi ya dhamana ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mfanyabiashara Yusufali Maji (41) na wenzake watatu.
Manji na wenzake, pia wanakabiliwa na kukutwa na vitambaa vya sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo amefungua maombi yaliyosajiliwa kwa namba 122/2017, kupinga hati iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuzuia dhamana dhidi yake na yalitajwa jana mbele ya Jaji Isaya Arufani.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Paul Kadushi, Simon Wankyo na Tulumanywa Majigo, ulidai mahakamani kwamba wanaomba muda kwa sababu wana nia ya kuwasilisha pingamizi la kupinga maombi ya utetezi.
Pia, ulidai kuwa wanaomba mahakama iwape muda wa kuwasilisha majibu ya hati ya maombi ya mshtakiwa.
Jaji Arufani alisema upande wa Jamhuri uwasilishe majibu na pingamizi lao Agosti Mosi na upande wa utetezi kama watakuwa na majibu ya nyongeza wawasilishe Agosti 2 na mahakama hiyo itasikiliza maombi hayo Agosti 4, mwaka huu.
Katika maombi hayo, Manji anaiomba Mahakama Kuu kutengua hati ya DPP ya kuzuia dhamana yake iliyowasilishwa Julai 5, mwaka huu aliposomewa mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na sare hizo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU
yaani makala yote MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/manji-kuomba-dhamana-mahakama-kuu.html
0 Response to "MANJI KUOMBA DHAMANA MAHAKAMA KUU"
Post a Comment