title : Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora
kiungo : Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora
Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora iliyoandaliwa chini ya mpango wa APRM kwa Tanzania, ambapo Tanzania imesifika kuwa kudumisha amani na umoja pia kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50.
Akizungumza katika mkutano wa na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania Rehema Twalibu akiambatana na Mjumbe wa wa Jopo la Watu Mashuhuri na Kiongozi wa Mchakato wa Tanzania Dkt. Rachel Mukamanana alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika kesho Julai 19, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam, ambapo Makamu wa Rais Mh. Samia Hassan Suluhu atazindua ripoti hiyo.
Rehema alisema kuwa lengo la APRM ni kuzisaidia nchi za kiafrika, Tanzania ikiwa mwanachama mmojawapo, kuhakikisha kuwa zinaimarisha utawala bora. Hii ni kwa kuwashirikisha wananchi wao kubanisha changamoto ili kuzigeuza kuwa fursa za maendeleo na mambo mazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchi yenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.
Aidha, katika ripoti ya mwaka 2012 ilibainisha sifa hizo kwa Tanzania za kudumisha amani na umoja pia kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50, pamoja na uboreshwaji wa utoaji huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, usawa wa kijinsia na Teknolojia na habari na mawasiliano (TEHAMA).
Alibainisha sifa zingine kwa Tanzania “kuwa ni kulinda haki binadamu, matumizi ya lugha moja ya kiswahili, na hatua za maendeleo ya kiuchumi nchini”
Katibu huyo alisema kuwa uzinduzi wa ripoti ni utekelezaji wa mojawapo ya matakwa ya kiutaratibu katika mchakato wa APRM, ikiwa ni kiashiria kimojawapo cha utekelezaji rasmi ya yale yaliyoandikwa kwenye ripoti pia kielelezo cha utayari wa Serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.
Akizitaja changamoto zinazoikabili Tanzania kutokana na ripoti ya mwaka 2012, Katibu Mtendaji huyo wa APRM Tanzania alisema kuwa “ katika masuala ya demokrasia na siasa, hakuna Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwa viongozi wake ni wateule wa Rais, Taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa bado hazina meno ya kutosha katika kudhibiti rushwa nchini, na kumekuwepo na migogogro ya ardhi kati ya wazawa na wawekezaji ambapo baadhi ya wawekezaji wamekuwa wakihodhi ardhi za wazawa bila kutoa fidia kwa wakati wala kuwapatia maeneo mbadala” .
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Tathimini za Nchi katika Sekretarieti ya APRM na Mratibu wa Mchakato wa Tananzia Dkt. Rachel Mukamunana alisema kuwa wanatarajia kuona Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ikipatia ufumbuzi changamoto zilizoainishwa katika ripori ya mwaka 2012.
APRM Tanzania ilipewa dhamana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia majukumu ya nchi katika kuratibu tathimini ya Utawala bora kwa mujibu wa wa miongozi ya Wakuu wa Nchi za Kiafrika.
Hivyo makala Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora
yaani makala yote Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-kuzindua-ripoti-ya.html
0 Response to "Makamu wa Rais kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora"
Post a Comment