KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
kiungo : KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

soma pia


KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Na Robert Hokororo

Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata za Lagana, Itilima na Talaga. Katika ziara hiyo wajumbe hao pamoja na wataalamu kutoka halmashauri walitembelea maendeleo ya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mwadulu iliyopo kata ya Lagana.

Wakiwa eneo hilo wajumbe hao kupitia kwa mwenyekiti wa halmashauri, Boniphace Butondo walipongeza juhudi za uongozi wa shule hiyo kwa ubunifu na kutumia vizuri fedha za Serikali.

Butondo aliwataka wanakamati ya shule kuendelea kuupa ushirikiano uongozi wa shule hiyo ili waendelee kushughulikia shughuli za maendeleo kupitia mpango wa elimu bure. Kamati hiyo iliweza pia kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Lagana ambayo inajengwa kwa nguvu ya wananchi ambapo walihimiza waendelee kuchangia.

Ziara hiyo pia ijumuisha kata ya Itilima ambapo wajumbe na wataalamu hao walikagua ujenzi wa vyumba viwili vya darasa shule ya msingi Ipililo pamoja na kata ya Talaga ukarabati wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Nhobola.

Waliridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi huo ambapo walimpongeza afisa elimu ufundi, Moshi Balele kwa kufuatilia kwa ukaribu shughuli zote zinazoendelea.

Hiyo ni mojawapo ya ziara za kukagua miradi ya maendeleo zinazofanywa na kamati mbalimbali za Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiongozana na mchumi kutoka halmashauri hiyo, Veronica Massawe katika kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiwaelekeza jambo mafundi waliokutwa na kamati wakiendelea na shughuli ya kusakafia mojawapo ya vyumba vya madarasa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa mojawapo ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lagana wakati wa ziara hiyo.
Ofisa elimu ufundi, Moshi Balele akiwaelekeza wajumbe wa kamati namna ujenzi wa chumba cha darasa unavyoendelea katika shule ya msingi Ipililo.
Chumba cha darasa katika shule ya msingi Mwamadulu ata ya Lagana kikiwa katika hatua mwisho wa ujenzi wake.


Hivyo makala KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

yaani makala yote KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/kamati-ya-fedha-kishapu-yafanya-ziara.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO"

Post a Comment