DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM

DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM
kiungo : DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM

soma pia


DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM

Na Jumbe Ismailly -HANANG . 

ALIYEKUWA diwani wa kata ya Gihandu,wilayani Hanang,Mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo,Mathayo Samuhenda amejiuzulu udiwani wa kata hiyo na kujiunga na Chama Chama Mapinduzi (CCM)

Akitangaza azma yake hiyo ya kujiuzulu katika nafasi yake ya udiwani wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Gihandu,Samuhenda alisisitiza kwamba aliamua kujiuzulu na kuwaacha wapiga kura wake siyo kwa njia ya ukatili bali alifikia maamuzi hayo kwa lengo la kuwaunganisha wananchi wote wa kata hiyo.  

Aidha alifafanua kwamba katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa wananchi wa kata hiyo wana matatizo ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kutokana na wanasiasa kutumia mtaji huo kuomba kura.
“Inatosha wanasiasa sisi tutumie shida ya maji ili tuoate kura tuondoke,inatosha..na watu wa Gihandu nawaomba sana hiyo ikiletwa kama sehemu ya mnada mzuri tu wa mtu kujinadi mkataeni inatosha tumeumia vya kutosha.”alisisitiza Samuhenda. 

Hata hivyo diwani huyo aliyejiuzulu aliweka bayana kwamba umefika wakati sasa kwa wanasiasa kubadili ajenda za kupatia kura za Gihandu na isiwe upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwani hiyo sasa imekuwa ni kejeli

Akimpokea diwani huyo,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoendeleza makundi licha ya kuwa hivi sasa siyo wakati wa kumpeni na badala yake aliwataka kuvunja makundi hayo na kusisitiza juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
 Ni Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,DK.Mary Nagu (wa kwanza kutoka kushoto) akimpongeza aliyekuwa diwani wa Kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda mara baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu akipokea kadi ya Chama Cha ACT Wazalebdo kutoka kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda.
 Aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu kwa tiketi ya ACT Wazalendo,MATHAYO SEMUHENDA akipokea kadi ya CCM baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
 baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya na Mkoa wa Manyara wakishiriki kikamilifu pamoja na wanachama wapya kula kiapo cha uadilifu baada ya kuwakabidhi kadi za chama wanachama wapya wa chama hicho.



Hivyo makala DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM

yaani makala yote DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/diwani-act-wazalendo-kata-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM"

Post a Comment