title : Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao
kiungo : Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao
Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeambiwa Mfanyabiashara Yusufali Manji (41) bado anaumwa na yuko kwenye matibabu katika hospitali ya gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salam.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Bw. Nassoro Katuga amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa.
Amedai kuwa, kesi hiyo leo ilikuja kwa kutajwa lakini Upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 4, mwaka huu.
Katika kesi hiyo Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa.
Katika Mashtaka hayo, wanadaiwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya milioni 195.5 na mihuri ya JWTZ na magari ya serikali kinyume cha sheria.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa kampuni ya Quality Group Deogratius Kisinda(28), mtunza stoo Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43) mkazi wa Chanika.
Mfanyabiashara Yusufali Manji
Hivyo makala Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao
yaani makala yote Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/hali-ya-yusuf-manji-bado-tete-kesi-yake.html
0 Response to "Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao"
Post a Comment