RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI

RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI
kiungo : RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI

soma pia


RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda jana Alhamisi June 1, 2017 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.

Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo  Mhe Paul C. makonda  amesema kuwa jumla ya Miradi 40 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam yenye thamani ya Shilingi 244,392,530,334 huku akibainisha kuwa Miradi 12 imezinduliwa, Miradi 15 imewekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili imefunguliwa na Miradi 11 imetembelewa.

Rc Makonda alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo , uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 wenye kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu pia umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya jitihada ya kudhibiti ni ajenda muhimu kwa mustakabali wa maisha ya mtanzania kwa kuwa linagusa nguvu kazi ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akitoa taarifa ya Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
Baadhi ya Wananchi waliozuru katika dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakifatilia dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017.



Hivyo makala RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI

yaani makala yote RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/rc-paul-makonda-amkabidhi-mwenge-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU RC NDIKILO WA PWANI"

Post a Comment