title : PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA
kiungo : PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA
PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Gabriel Silayo alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo watumishi wa umma ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili hatimaye wastaafu kwa amani.
“Na kwa kufanikisha hilo, tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo washirika wetu, SIDO, na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao watatoa elimu ya namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha Bw. Silayo.
Bw. Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili wawaelimishe jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya kustaafu utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo linawezekana.” Alisema
Alisema semina hiyo itakuwa ya siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi Juni 2, 2017.
Zaidi ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza wanahudhuria semina hiyo ya mafunzo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo
Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa
Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza
Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli.
Hivyo makala PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA
yaani makala yote PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/pspf-yawapiga-msasa-wastaafu-watarajiwa.html
0 Response to "PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA"
Post a Comment