title : Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba
kiungo : Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba
Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amekabidhi jumla ya vifaa 831 vyenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 400, kwa kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjini, vifaa vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Silvestry Koka.
Awali kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua maeneo ya majengo ya Kituo hicho cha Afya huku akbaini mambo mbalimbali aliyoagiza yafanyiwe kazi ili kituo hicho kiweze kuwa Hospitali ya Wilaya pindi itakapokamilisha vigezo
Wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za Mh. Koka kwa kujali wananchi wake kwani hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza kutumia maarifa na ukaribu wake na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa hivyo vitakuwa faraja kubwa kwa Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo jirani.
“Nampongeza Mbunge Koka kwa kuwaletea vifaa hivi. Kwani ni vizuri na vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kibaha na maeneo yake ya jirani. Nakupongeza sana sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo.
Aidha, aliwataka wananchi wa Kibaha mjini waweze kuwa karibu na Mbunge wao na wamwamini kwani anawajali ndio maana anawatumikia kwa kila njia ikiwemo kuwaletea maendeleo kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Silvestry Koka amemshukuru Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kuweza kufika na kujionea Kituo hicho sambamba na kukabidhi vifaa huku akimuomba kuendelea kufika mara kwa mara kujionea mipango ya Afya jimboni humo.
“Leo hiii najisikia faraja kwa vifaa hivi kuweza kufika hapa jimboni kwangu kutoka nchini Marekani. Nawaomba vitumike kwa uangalifu mkubwa sana na viweze kuwa msaada kwetu” alieleza Mh. Koka.
Awali alieleza kuwa, kiasi cha shilingi milioni 32 fedha zilizotolewa na Halmshauri ya mji wa Kibaha ziweza kusaidia usafirishaji wa vifaa hivyo kutoka nchini Marekani huku yeye kama Mbunge akitumia gharama ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya kuwaleta wataalam kwa ajili ya ukaguzi na kuvifunga vifaa hivyo.
Mbunge huyo ameeleza kuwa, vifaa hivyo vitagawia katika zahanati na vituo vyote vilivyopo mjini Kibaha na maeneo mengine yenye uhitaji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika tukio hilo la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhia nyaraka zenye vifaa tiba akikabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi nyaraka yenye idadi ya vitu hivyo vya vifaa tiba kwa uongozi wa Kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjin wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuhudia vitu hivyo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha wakati wa tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla kisalimiana na na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Kibaha
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni kwa ofisi ya Wilaya ya Kibaha
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya Madiwani wa Jimbo la Kibaha Mjini
Baadhi ya vifaa tiba vilivyokabodhiwa leo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akifanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya kituo cha Afya Mkoani
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mahabara katika kituo cha Afya Mkoani, Kibaha Mjini
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la Chumba cha Upasuaji katika kituo cha Afya Mkoani, Kibaha Mjini
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na mbunge wa jimbo hilo
Wakiangalia vifaa hivyo
Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Koka akielezea namna vifaa hivyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na baadhi ya watendahi wa Hospitali ya Mkoa, Kituo cha Afya Mkoani na Mganga Mkuu wa Mkoa
Hivyo makala Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba
yaani makala yote Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/dk-kigwangalla-ampongeza-mbunge-wa.html
0 Response to "Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba"
Post a Comment