title : Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696
kiungo : Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696
Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696
Frank Mvungi- Maelezo
Serikali imetumia shilingi bilioni 16.9 kununua vifaa vya maabara na vile vya wanafunzi wenye mahitaji maalum vitakavyonufaisha shule za sekondari 1696 ambapo shule 1625 ni za Kata na 71 ni kongwe ambazo kwa sasa zipo katika ukarabati.
Akihutubia wakati wa hafla ya kuzindua mpango wa kusambaza vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa inaboresha sekta ya elimu ili azma ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda itimie kwa kuwa Taifa litaweza kuzalisha wanasayansi kulingana na mahitaji.
“Tunatoa vifaa hivi kwa awamu ya kwanza kwa shule zilizokamilisha ujenzi wa maabara, hivyo ni matumaini yangu kuwa wale ambao hawajakamilisha watafanya hivyo ili awamu ijayo nao wapate vifaa hivi.” Alisisistiza Majaliwa.
Aliongeza kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha zaidi ya shule 4,000 nchini zinakuwa na vifaa vya maabara, walimu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na mazingira rafiki ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia kushiriki katika ujenzi wa Taifa.
Pia Waziri Mkuu ameonya kuwa Serikali itachukua hatua kali dhidi ya mtu yoyote atakaye sababisha mwanafunzi wa kike kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo ambapo atakabiliwa na adhabu ya kwenda jela miaka thelathini.
“Awe baba au mama au mtu yoyote ambaye itathibitika kuwa amemsababishia ujauzito mwanafunzi, adahabu yake ni kifungo cha miaka thelathini jela.” Alisisitiza Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhi moja ya kifaa cha kufundishia masomo ya sayansi kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Juhudi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akipata maelekezo toka kwa moja ya mwalimu wa masomo ya sayansi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696
yaani makala yote Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/bilioni-169-kunufaisha-sekondari-1696.html
0 Response to "Bilioni 16.9/- kunufaisha sekondari 1696"
Post a Comment