title : KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO
kiungo : KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO
KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO
Mradi huo umezinduliwa na taasisi tatu za Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation katika sherehe zilizohudhuriwa na maofisa wa serikali, wawakilishi wa vyama vya wakulima, taasisi za fedha, kampuni za mbegu, wafanyabiashara wa nyenzo za kilimo na wale wanaojishughulisha na biashara za mazao ya sekta ya kilimo.
Kifaa hicho cha dijitali kitawawezesha wakulima kulipia mapema pembejeo wanazohitaji kupitia simu za mkononi kwa bei nafuu. Pia kifaa hicho kitawapa wakulima pembejeo kulingana na mazao na malengo yao ya uzalishaji na pia kupata taarifa za ushauri kuhusu matumizi bora ya pembejeo hizo.
“Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni kwamba hukosa fedha mwanzoni mwa msimu wa upandaji mazao, jambo ambalo huwalazimisha kutafuta fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo na hivyo kuwaongezea mzigo,” alisema Hedwig Siewertsen, kiongozi anayeshughulikia masuala ya fedha wa shirika la Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA).
“Kifaa hicho cha dijitali kwa ajili kusaidia upatikanaji pembejeo za kilimo ni ufumbuzi wa kipekee. Kitawaimarisha na kuwasaidia wakulima kutenga fedha kwenye akaunti zao za simu ili waweze kununua pembejeo bora kwa muda muafaka na kwa bei nafuu ya asilimia 30.”
Wakulima wadogo nchini Tanzania huzalisha asimia 70 ya chakula ingawa karibu nusu yao hawazalishi chakula cha kutosha kwa ajili ya mauzo. Wanakabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya kilimo cha kisasa, hawana uwezo wa kujipatia pembejeo bora na wanakosa huduma za kiufundi za ughani zinazoweza kuwasidia kukuza kilimo pamoja na ukosefu wa mafunzo.
Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Badala yake wakulima hawa wanategemea zaidi kilimo cha mvua, zana duni za kilimo na mbegu hafifu ambazo ubora wake hupungua kila msimu wa kilimo.
Hivyo makala KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO
yaani makala yote KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/kifaa-cha-dijitali-kuwawezesha-wakulima_30.html
0 Response to "KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO"
Post a Comment