Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi

Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi
kiungo : Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi

soma pia


Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi

Na Husna Saidi- MAELEZO

Takribani shilingi milioni 271 zinadaiwa kwa wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini, Mkoani Mara ikiwa ni kodi ya Pango la Ardhi. 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipofanya ukaguzi wa mfumo wa kodi ya ardhi hivi karibuni Mkoani humo.

Waziri Lukuvi alisema kuwa amekagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Musoma mjini ili kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi nchini wanalipa kodi kwa hiari kabla ya hatua za kisheria hazijafuata dhidi yao.

“Nimeagiza kesi za madai ya kodi zitolewe hukumu ndani ya siku moja tu ili wadaiwa waweze kuchukuliwa hatua ya kuuzwa kwa mali zao haraka”, alisema Lukuvi.

Aidha Waziri Lukuvi alimtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Musoma Bw.Joseph Kamonga kuwasilisha majina ya wadaiwa hao katika Mahakama ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupiga mnada majengo na mali zao kama wakikaidi kulipa kodi hiyo.

Kwa upande mwingine Lukuvi alifanya uzinduzi wa mpango kabambe (Master Plan) wa Manispaa ya Musoma na kuwapongeza viongozi na watendaji wa Manispaa hiyo kwa kuwa Manispaa ya kwanza nchini kuweza kuzindua mpango huo kutumia kampuni za ndani katika utekelezaji wa mpango huo.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Lukuvi amezitaka Manispaa nyingine kutumia kampuni za ndani ya nchi ambazo zimesajiliwa na Wizara ya Ardhi katika kutekeleza mipango mbalimbali ya ulipaji kodi za ardhi. 

Pia Waziri Lukuvi aliiagiza Manispaa ya Musoma kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa mpango kabambe kwa kutumia wataalam wao (wa serikali) au Makampuni ya ndani na kutoa nakala za kutosha ili mpango huo uwafikie wadau wote na kutaka mpango huo utafsiriwe kwa Kiswahili ili Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waweze kuwafikishia wananchi kwa urahisi.


Hivyo makala Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi

yaani makala yote Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/wakazi-wa-manispaa-ya-musoma-mjini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini Wadaiwa Mil. 271 za Kodi ya Ardhi"

Post a Comment