SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA

SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA
kiungo : SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA

soma pia


SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA


KIJAJI
Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma
Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi  wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo  hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.
Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaluum (CCM) Arusha, Mhe. Catherine Magige aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa mafao waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo.
Mhe. Magige aliliambia Bunge kuwa waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambao waliachishwa kazi mwaka 2000, hawajalipwa mafao yao hadi sasa.
Akijibu swali hilo, Dkt. Kijaji alisema kuwa katika zoezi la ulipaji wa mafao kwa wafanyakazi hao Serikali ililipa Sh. 217,366,296 mwezi Januari, 2000 ambapo baadae walipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao kuwa wamepunjwa.
“Serikali baada ya kupokea malalamiko hayo, ilihakiki na baada ya kujiridhisha mwezi Agosti, 2000, ilitoa idhini ya kulipa tena kiasi cha Sh. 273, 816, 703 kwa ajili ya mapunjo ya mishahara na mafao ya wafanyakazi hao” aliongeza.
Hata hivyo, Mhe. Magige hakuridhishwa na majibu ya Dkt. Kijaji na alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza alisema kuwa Serikali imewalipa wafanyakazi hao awamu ya kwanza tu na hawakupewa nyongeza yoyote licha ya kuwasilisha malalamiko hayo.
Mhe. Magige aliongeza kuwa Wizara ya Fedha ilishawahi kwenda kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu, na Serikali iliipa jukumu la kusimamia malipo hayo Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo mpaka sasa bado haijalipa.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (MB), Mhe. Ramo Makani aliliomba Bunge limpe muda wa kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili aweze kutoa majibu sahihi.


Hivyo makala SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA

yaani makala yote SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/serikali-haidaiwi-na-wafanyakazi-wa_19.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA"

Post a Comment