title : WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI
kiungo : WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI
WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI

Maandamano ya wafanyakazi kama yanavyoonekana pichani Jijiji Arusha.
Maandamano yakiendelea kuelekea katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Karume Jijiji Arusha.
Na Vero Ignatus,Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta amekenea vikali tabia ya baadhi ya Waajiri wakorofi wanaowanyanyasa Wafanyakazi wao na kuwataka Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuwachukulia hatua mapema pale watakapobainika.
Amesema hayo wakati akitubia katika Siku ya Wafanyakazi mkoani Arusha akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo Mrisho Gambo ambapo amewataka waajiri wajiepushe na vitendo vya unyanyasaji kwani sheria itafuata mkondo wake.
"Hatutamfumbia macho baadhi ya waajiri wakorofi wanaowanyanyasa wafanyakazi wao vyama vyavwafanyakazi fanyeni jitihada kuwabaini ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.alisema Kimanta.''
Mhe.Kimanta amewataka Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kutatua kero za wafanyakazi badala ya kusubiri siku ya wafanyakazi na kutoa kero zao.
Nae Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya Wafanyakazi mkoani Arusha (TUCTA) Lota Laizer ameiomba serikali itoe nyongeza ya mishahara pamoja na ongezeko la asilimia la 1 la kila mwaka kama ilivyo matakwa ya sheria.
Aidha Laizer amewataka Wafanyakazi kuwa viongozi wa kisiasa wanatekeleza majukumu yao bila kukiuka sheria za wafanyakazi na kutumia lugha za kuwadhalilisha wafanyakazi.
Hivyo makala WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI
yaani makala yote WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/05/waajiri-waaswa-kutowanyanyasa.html
0 Response to "WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI"
Post a Comment