WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA

WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA
kiungo : WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA

soma pia


WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA



Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mlango (geti) la kielektroniki kwa ajili ya ukaguzi wa abiria, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Watalii kutoka Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kutoka kushoto ni Naomi Moscovich, akiwa na binti zake, Dana Moscovich(kulia) na Lihi Moscovich (katikati). Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
…………………………………………………………………….

*Ni yenye kuonyesha wanyama, milima, fukwe, mambo ya utamaduni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa bodi ya KADCO uhakikishe unaweka mabango ya kielektroniki yenye kuonesha vivutio vya utalii kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

 “KADCO na Wizara ya Maliasili na Utalii, shirikianeni kuweka utaratibu wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii hasa wanyama kwenye viwanja vyote vya ndege. Tunazo mbuga, milima, fukwe za bahari na ngoma za makabila mbalimbali, wekeni mabango yanayobadilisha picha.” 

 “Screens zenye wanyama wanaobadilikabadilika zinaleta mvuto lakini pia ni fursa ya kutangaza vivutio vyetu. Nimezunguka humu ndani, kuta zote ni nyeupe tu, tumieni fursa hiyo kutangaza tamaduni zetu na vivutio tulivyonavyo,” Waziri Mkuu alimweleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), Mhandisi Christopher Mukoma. 

Alitoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Aprili 27, 2019) wakati akikagua miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwaaga watalii 274 kutoka Israeli wanaowawakilisha wenzao 1,000 walioondoka nchini jana kurejea kwao.

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili, sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.
Pia alimwagiza Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji kwenye kiwanja hicho cha ndege, Bw. Filbert Ndege awasiliane na makao makuu yake ili waangalie uwezekano wa kuongeza madirisha ya kutolea huduma za uhamiaji (counters) ili huduma hiyo itolewe kwa kasi zaidi. 

 “Angalieni cha kufanya, ikibidi eneo hili lipanuliwe na counters nyingine ziongezwe ili kufasttrack utoaji wa huduma hasa msimu ambao watalii wengi huingia nchini.”

 Pia aliwataka KADCO waboreshe eneo la maegesho ya magari kwa kufanya upanuzi na kujenga maturubai ya vivuli (shades) ili kuyakinga na jua kali magari ya wateja


Hivyo makala WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA

yaani makala yote WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/waziri-mkuu-aagiza-mabango-ya-utalii.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA"

Post a Comment