title : Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi
kiungo : Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi
Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, watu wanne wanaodaiwa kuuliwa na askari polisi Mkoani Kigoma wapo hai na watafika Mahakamani kutoa ushahidi.
Mpelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Maruru amedai hayo leo Aprili 24, 2019 wakati alipofika mahakamani hapo kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya uchochozi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambayo imeanza leo kusikilizwa.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, kutoa ushahidi wake, Mururu ambae ni shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri amedai kwatu hao wanne ambao Zitto alidai kuwa walikuwa majeruhi na kupelekwa kituo cha afya Nguruka, na kwamba polisi waliwachukua na kuwaua sio kweli kwani watu hao wanne pamoja na Mganga wa Kituo cha Afya Nguruka, watakuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, amedai, Oktoba 28, mwaka huu Zitto akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alitoa maneno ya uchochezi ambayo yamesababisha kuwachonganisha wananchi na jeshi la polisi kwamba sio watumishi bali ni wauaji wa wananchi.
Maruru amedai baada ya taarifa hiyo walianza kufuatilia kwa kina ikiwemo kuwasiliana na SSP Mark Njela wa Kigoma ili wapate kujua hali ikoje kama ilivyotamkwa na Zitto ambapo SSP Njela alimwambia kuwa mambo yaliyosemwa ni ya uongo na dhamira ni kuchonganisha jeshi na wananchi kwani katika kufuatilia taarifa hiyo, alienda maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam na kukuta wananchi wakijadiliana kuhusu taarifa iliyotolewa na Zitto na kwamba walionesha kuchukizwa na taarifa hiyo.
Amedai, kufutia hayo, alirudi ofisini na kuwaita makachero wazoefu na maofisa wa makosa ya mtandao ili kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na tulipeana majukumu ikiwemo kufuatilia na kukusanya ushahidi kuhusu tuhuma hizo na kuitisha mashahidi.’’ alisisitiza.
Aliendelea kudai kuwa kauli zilizotoka kwenye nakala ya taarifa kwa vyombo vya habari ilionesha kuwa jeshi hilo ni wauaji kwani Zitto alisema ‘Polisi wameenda kituo cha afya Nguruka na wamewachukua majeruhi wanne waliopelekwa na kuwaua’.
Pia katika taarifa hiyo ilionesha ‘polisi wakiwa kwenye operesheni hiyo wameua watu wengi sana’. Maruru alidai kwamba maneno hayo ni ya uchochezi na yanalenga kuwachonganisha na wananchi.
Shahidi huyo alidai kitengo cha makosa ya mtandao walifanikiwa kupata ushahidi wa video na walimkamata mshitakiwa na walipompekuwa walimkuta na taarifa kwa vyombo vya habari.
Katika kesi hiyo, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2019 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki
Anadaiwa kusema, watu waliokuwa ni majeruni katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, Polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospital kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua".
Hivyo makala Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi
yaani makala yote Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/waliodaiwa-kufa-sasa-kuibukia.html
0 Response to "Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi"
Post a Comment