title : Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu
kiungo : Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu
Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeweka utaratibu wa kutembelea Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule za Sekondari ili kutoa elimu ya namna ya kuomba Mikopo katika Bodi hiyo.
Akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic Afisa Mwandamizi Bodi hiyo Josephat Bwathondi amesema kuwa bodi iko kwa kazi moja ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji kwa ajili ya elimu ya juu ambapo kukosekana kwa chombo hicho baadhi ya watanzania wangekosa elimu ya juice kutokana uchumi walio nao.
Amesema kuwa lengo la kuwafikia Wanafunzi wa shule hiyo ni kwa ajili ya kuwapa namna ya uombaji mikopo na taarifa zinazohitajika katika uambaji mikopo.
Aidha amesema taarifa za msingi katika maombi hayo ni vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi, Wazazi, Kama mwanafunzi kafiwa na mzazi kuwepo kwa cheti cha kifo katoka kwa Wakala wa Udhamini, Ufilisi, Usajili wa Vifo na Vizazi (RITA).
Amesema utaratibu hapo nyuma haukuwepo lakini wameona ni muda mwafaka wa kutoa elimu ya uoambaji Mikopo.
Nae Afisa wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi hiyo Emmanuel Mtavangu amesema kuwa katika kuwapa elimu ya uombaji Mikopo pia lazima watambue kuwa Mikopo hiyo inarejeshwa kwa ajili ya kusomesha wahitaji wengine.
Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Josephat Bwathondi akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ubungo Islamic wakati walipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi Wasichana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic wakisikiliza mada za Bodi ya Mikopo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Sekondari hiyo.
Wanafunzi Wavulana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic wakisikiliza mada za Bodi ya Mikopo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Sekondari hiyo.
Afisa wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Emmanuel Mtavangu akitoa maelezo ya taratibu za Urejeshaji mikopo baada ya kuhitimu shahada ya kwanza wakati Bodi ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu
yaani makala yote Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/ubungo-islamic-wapata-elimu-ya-kuomba.html
0 Response to "Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu"
Post a Comment