TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao

TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao
kiungo : TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao

soma pia


TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao

Na Karama Kenyunko, Blobu ya Jamii
WAFANYABIASHARA wa kampuni kubwa za mafuta na gesi wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuendelea mchakato wa  mradi wa kuchakata gesi na mafuta mkoani Mtwara kwa sababu hadi sasa hakuna kinachoendelea.

Pia wametaja changamoto nyingine inayokabili sekta hiyo ni kuhusu mikataba yao ya makubaliano ya uzalishaji na mauzo ya gesi na mafuta ambayo serikali iliichukua ili kuiangalia upya lakini hadi sasa haijairudisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania  (TPSF) Godfrey Simbeye, amebainisha hayo leo Aprili 4, 2019  jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliyokutanisha kampuni kubwa za uwekezaji wa mafuta na gesi zaidi ya 30 kujadili changamoto walizonazo ili ziwasilishwe serikalini kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.

Simbeye amesema walikutana na wafanyabiashara hao na moja ya changamoto waliowaeleza ni kutoona dalili zozote za kuanza kwa mradi huo wa gesi mkoani Mtwara ambao wanaamini ukianza utawanufaisha watu wengi. 

Kuhusu mikataba alisema wafanyabiashara hao wameomba Serikali iwarejeshee kwa sababu muda mrefu umepita tangu iichukua kwa ajili ya kuikagua.

"Mikataba hii ilichukuliwa na Serikali ili ikaguliwe ila mpaka sasa ni muda mrefu bado hawajairudisha jambo ambalo linakwamisha baadhi ya shughuli wanazozifanya hivyo wafanyabiashara wanaiomba na kuhimiza  serikali iwarejeshe mikataba hiyo.

TPSF ilikutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kutueleza kuwa hadi mwishoni mwa mwezi huu watakuwa wameshakamilisha zoezi la kupitia mikataba hiyo hivyo tunasubiri kuona Kama ahadi hii itakuwa ya kweli, " alisema.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya TPSF,  balozi Abdulsamand Abdulrahim amesema wamewaita wadau hao ili waweze kuwapatia mrejesho wa kazi za miezi mitano zilizofanywa na bodi hiyo  hasa zile za kukutana na Serikali ili kuwasilisha changamoto za wafanyabiashara ili kuweza kuisaidia sekta ya mafuta na gesi.

Amesema, walishakutana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na aliyekuwa Waziri wa Madini Angela Kairuki kwa vipindi tofauti na pia wamefanya mkutano mkubwa na dialogue  baina ya AG na bodi ya TPSF  kuwawasilishia chagamoto zinazozikabili sekta binafsi na wafanyabiashara.

Amesema,  miongoni mwa kero wanazokutana nazo ni namna ambavyo wafabyabiashara wanasumbuliwa na TRA katika ulipaji kodi  na baadhi viongozi ambao wanakwenda kukaa na kuwasumbua wawekezaji wakati hawana mamlaka  ya kufanya hivyo.
 MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye (aliyesimama)akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha makampuni makubwa ya wawekezaji sekta ya mafuta na gesi zaidi ya 30 kujadili changamoto walizonazo ili ziwasilishwe serikalini kwa ajili yakutafutiwa ufumbuzi. Mkutano huo umefanyika leo Aprili 4,2019 jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi, (TPSF), Balozi Abdulsamad Abdulrahimu ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa chama cha watoa huduma sekta ya gesi na mafuta akizungumza wakati wa mkutano  uliokutanisha makampuni makubwa ya wawekezaji katika sekta ya Mafuta na gesi zaidi ya 30  ya  mafuta nchini kwa lengo la kujadili  changamoto walizonazo ili ziwasilishwe serikalini kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
Mkurugenzi mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na anayesikiliza pembeni ni Mjumbe wa bodi TPSF Balozi Abdulsamad Abdulrahimu ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa chama cha watoa huduma sekta yagesi na mafuta.


Hivyo makala TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao

yaani makala yote TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/tpsf-yakutanisha-kampuni-za-mafuta-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TPSF yakutanisha kampuni za Mafuta na Gesi kujadili changamoto zao"

Post a Comment