title : SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA
kiungo : SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA
SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.
Sherehe za Kumuaga Mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mhe. Jasson Rweikiza zimefanyika Jana katika viwanja vya Shule za Rweikiza zilizopo Maeneo ya Kyetema Bukoba.
Sherehe hizo zilizofanyika mnamo Aprili 23, 2019 zikiwa zimehudhuliwa na watu zaidi ya 5000 wakiwemo Viongozi wa Dini, Serikali, Chama Tawala, Madiwani, watumishi wa serikali, wananchi kutoka Kata zinazounda Halmashauri ya Bukoba na wengine kutoka nje ya Mkoa wa Kagera.
Kivutio kikubwa katika sherehe hiyo ni Mshereheshaji wa shughuli mbali mbali za Kitaifa Ndg. Mavunde akionyesha umahiri mkubwa wa kuongoza shughuli aina zote na akiacha waalikwa wakiumwa mbavu kwa Vicheko.
Miongoni mwa wasanii waliotoa burudani ni pamoja na Saida Karoli aliyetamba kwa kibao maalum cha "Obugenyi" kinachofanya vizuri sana katika sherehe za Harusi.
Familia ya bibi harusi wakiongozwa na Baba na Mama Mzazi wakati wakiingia Ukumbini katika Sherehe ya Kumuaga Binti yao.
Mapema Viongozi mbali mbali wakiwasili katika Send off ya Hope Jasson Rweikiza, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro.
Pichani kushoto ni Mkurugenzi Wa Nyanza Bottling Co. Ltd Christopher Mwita Gachuma, akiwasili Ukumbini akisindikizwa Na Diwani Wa Kata ya Kaibanja Mh. Jasson Lwankomezi.
Wazazi wa Aloyce Kutoka Usukumani wakicheza Wimbo wa Kubyala wakisaidiwa na Mshereheshaji Bwn. Mavunde
Kikundi cha burudani (Brigthers) maarufu kama Kibeta One kikisafisha njia kabla ya maharusi kuingia Ukumbini.
Bi Harusi Mtarajiwa Hope Jasson Rwekiza akiingia ukumbini huku akicheza kufurahia siku yake, akisindikizwa na Ndugu yake.
Wanameremeta wapendanao hawa Aloyce na Hope ambao baadae watakuwa Mwili mmoja.
Karibu senene baba watoto mtarajiwa
Muonekano wa Keki Maalumu iliyoaandaliwa kwa ajili ya Hope Rweikiza
Pichani Mpambe wa Hope akimsaidia kuandaa keki kabla ya kukatwa
Burudani ya Saida Karoli ikamsababisha Mhe. Abdallah Bulembo (MB) kunyanyuka akisindikizwa na Mbuge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Rweikiza, kuongoza wageni waalikwa kwenda kutunza.
Mama mzazi wa Hope, Bi. Stella akicheza ngoma ya Saida Karoli pamoja na Mwenyekiti wa Wazee Mzee Sadru Nyangasha.
Bibi Harusi mtarajiwa Hope akigonga glasi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Mama Buhiye wakati wa sherehe za Kumuaga zilizofanyika katika shule za Rweikiza Bukoba.
Pichani Mh. Rweikiza akitoa neno lake kwa bintiye kikubwa akiwa amemuusia Upendo na Kumcha Mungu.
Pichani Mh. Jasson Rweikiza (MB) akifurahi pamoja na Bintiye Hope Rweikiza katika sherehe ya Kumuaga Binti hiyo (send off).
Hivyo makala SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA
yaani makala yote SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/send-off-ya-binti-rweikiza-yavunja.html
0 Response to "SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA"
Post a Comment