TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII.

TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII.
kiungo : TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII.

soma pia


TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII.


Baadhi ya wachezaji mpira wakipata chakula ambacho kimeandaliwa na watoa huduma ya chakula (Mass food caterers).
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Watoa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko ya watu wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni bora za usafi ili kuhakikisha chakula kinachoandaliwa kinakuwa salama jambo ambalo litasaidia kulinda afya ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa mkutano wa watoa huduma ya chakula, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo,  amesema kuwa ni muhimu watoa huduma ya chakula kuzingatia sheria katika utendaji wao.

Kijo amesema kuwa uandaaji wa chakula pasipo kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni husababisha uchafuzi wa vimelea vya maradhi kwa watumiaji wa chakula hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chukula na Dawa (TFDA) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko ya Watu.

"Kama mtoa huduma wa chakuka hajazingatia usafi anaweza akasababisha madhara ya kiafya kama vile kuhara, kuhara damu, homa ya matumbo, minyoo pamoja na kipindupindu" amesema Kijo.

Amesema kuwa wakati umefika watoa huduma ya chakula wakatambua madhara yanayosababishwa na uchafuzi wa vimelea katika chakula kwani yameendelea kuwa tatizo kwa afya ya jamii.

Ameeleza kuwa uwepo wa magonjwa yanayotokana na kula chakula kisicho salama inatoa picha juu ya umuhimu wa kutoa kipaombele katika masuala ya usalama wa chakula.

"Utoaji wa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko ya watu inatakiwa kuzingatia matakwa ya sheria" amesema Kijo.

Kijo amefafanua kuwa sasa kuna ongezeko la watu wanatoa huduma ya chakula katika mikusanyiko ikiwemo misiba, mikutano, maofisini pamoja na sherehe mbalimbali hivyo vema kila mmoja akafata sheria.

"Kupitia mkutano huu watoa huduma wa chakula watapa fursa ya kufahamu taratibu za kupata kibali pamoja na kutoa mapendekezo yao ili kuimarisha usalama wa chakula wanachoandaa" amesema Kijo.

Katika hatua nyengine amebainisha kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kupitia TFDA inatendelea kushirikiana na watoa huduma ya chakula ili kulinda afya ya jamii.

Kwa upande wa watoa huduma ya Chakula kwenye mikusanyiko wemeonesha nia ya kushirikiana na TFDA katika kuboresha huduma zao kwa kuzingatia sheria.
Mkurungenzi wa Kampuni ya Love Catering Services inayotoa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko ya watu Michael Lee, amesema kuwa ni vizuri watu wakato huduma ya chakula kwa kufata utaratibu.

Amesema ni jambo njema ambalo TFDA wamelifanya kwa kutukutanisha leo katika mikutano huu ambao ni rafiki kwetu katika kutoa mapendekezo yetu kwa lengo la kujenga.

Hata hivyo Lee amebainisha kuwa watanzania wanapaswa kuheshimu kazi ya kupika chakula kwani taaluma kama zilivyo taalumu nyengine kwa baadhi ya watu wamekuwa wakifanya  wakitoa huduma ya chakula pasipo kufata utaratibu.

"Wapo ambao wanasoma taaluma ya mapishi kwa muda wa miaka minne ambapo sawa na taalamu nyengine ambazo zinatumia muda wa miaka hiyo hadi mimaliza Masomo" amesema Lee.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 20I5 zinabainikwa inakadiriwa watu milioni 600 kila mwaka  huugua kutokana na kula chakula kisicho salama.
Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Mamlaka ya Chakula Na Dawa (TFDA) Justin Makisi akizungmzia madhumuni ya mkutano wa wadau wanaotoa huduma ya Chakula uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya WHO inaeeleza kuwa kati ya watu milioni 600 wanaougua, watu 420, 000 hufariki dunia.

Tatizo la chakula kisicho salama barani afrika ni kubwa, kwani watu zaidi ya milioni 9I wanakadiriwa kuugua na I37,000 hufariki kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama.

Magonjwa ya kuhara uchangia asilimia asilimia 70 ya magonjwa yote yatokanayo na chakula katika bara la afrika.

Hapa Tanzania tumekuwa tukishuhudia watu wakiugua magonjwa mbalimbali kama vile homa ya matumbo (typhoid), minyoo, kuhara damu, kipindupindu huku wengine wakipoteza maisha.


Hivyo makala TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII.

yaani makala yote TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tfda-yawakutanisha-watoa-huduma-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TFDA YAWAKUTANISHA WATOA HUDUMA YA CHAKULA KUJADILI USALAMA WA AFYA YA JAMII."

Post a Comment