title : NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.
kiungo : NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.
NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa kuomba nafasi ya ajira katika Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.
Nafasi hiyo ni Afisa Rasilimali Watu Msaidizi atakayefanya kazi katika kitengo cha Rasilimali Watu na Usimamizi wa Miundombinu. Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hiyo ya ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti http://thecommonwealth.org.jobs.
Kwa kuzingatia sera ya Jumuiya ya Madola ya usawa wa kijinsia, Sekretarieti ya taasisi hiyo inawahimiza wanawake wengi zaidi wenye vigezo kuomba nafasi hizo. Mchakato wa kumpitisha mtaradhia wa nafasi hiyo utazingatia uwiano wa kikanda hususan kwa nafasi za maafisa waandamizi.
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo ni Ijumaa tarehe 12 Aprili, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
4 Aprili, 2019.
Hivyo makala NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.
yaani makala yote NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/nafasi-ya-ajira-katika-jumuiya-ya.html
0 Response to "NAFASI YA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA."
Post a Comment