title : KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA
kiungo : KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA
KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA
* Atoa milioni kumi kuendesha ofisi za wajane na kuhaidi kujenga ofisi za wajane makao makuu Dar
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa atachukua takwimu za matatizo ya wajane wa Mkoa huo na kumkabidhi Waziri wa Sheria na Katiba ambaye atamkabidhi jaji Mkuu ili matatizo hayo yaweze kushughulikiwa ndani ya miezi mitatu.
Akizungumza katika kongamano lililolenga kutatua kero za wajane katika masuala ya mirathi, uchumi na malezi Makonda amesema kuwa baada ya kukutana na wanawake na watoto waliotelekezwa mwaka uliopita matatizo mengi zaidi yaligundulika na kumpa uthubutu wa kuendelea mbele zaidi.
Amesema kuwa moja ya kitu wanachotarajia ni pamoja na kuweka mifumo bora na endelevu ya uongozi ili kuviepusha vizazi vijavyo na matatizo haya yanayojitokeza sasa.
Amesema kupitia kongamano hilo ataangalia mfumo wa sheria ambao utawasaidia wao na wengine huko mbeleni huku akisema katika suala la uchumi lazima akina mama hao watambue haki yao ya asilimia 4 ya fedha iliyotengwa na Serikali ambayo hutolewa bila riba na katika sekta ya malezi Makonda amesema kuwa kuna wataalamu watakaoshirikiana nao katika kupata ushauri juu ya namna bora ya kuwalea watoto wao ambao wengi wameharibikiwa kutokana na maendelea ya sayansi na teknolojia hasa katika mitandao ya kijamii.
Kwa upande wake katibu tawala wa Mkoa Abubakar Kunenge amewashukuru akina mama hao pamoja na wawezeshaji kwa kujitokeza kwa wingi huku akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuandaa kongamano hilo ambalo limelenga kutatua kero za mirathi,uchumi na malezi.
Akisoma taarifa Mwenyekiti wa kamati ya kuwasaidia watoto na wanawake wanaoishi kwenye mazingira magumu ambaye ni wakili wa kujitegemea na mshauri msaidizi wa masuala ya kisheria wa CCM Albert Msando amesema kuwa matokeo ya kampeni iliyoanzishwa na mkuu wa Mkoa iliyolenga kuwasaidia watoto na wanawake wanaoishi kwenye mazingira magumu wengi wa wazazi wa watoto hao ndio hao wajane waliojitokeza leo katika kongamano hilo, na amesema kuwa kamati hiyo ya watu 19 imegundua matatizo mengi kwa watoto hao ikiwemo kubakwa, kukosa haki za msingi, kunyanyaswa na kudhulumiwa huku utatuzi wa changamoto hiyo ni kubwa kuliko matatizo mengine.
Kwa upande mchungaji wa kanisa Anglican Mchungaji Daniel Mgogo amesema kuwa mamia wa wajane hao wamedhulumiwa na amewashauri viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya kata kusikiliza kero za aina hiyo huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa kwa hekima na uthubutu huo aliouonesha katika kuwasaidia wajane hao na kushauri kuwa suala la mirathi liwe sheria kwa kila mmoja kuandika mali na warithi wake ili kuwalinda wajane.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam, wasanii, wanasaikolojia, wawezeshaji, wanasheria pamoja na asasi 9 zisizo za kiserikali ambazo zimeshiriki katika kuwasaidia wajane hao kupata haki zao za kisheria kupitia kongamano hilo.
Mwimbaji wa taarabu Khadija Kopa akifurahi pamoja na akina mama wajane walioitikia mwito wa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika kongamano la utatuzi wa masuala ya mirathi, uchumi na malezi, leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajane waliohudhuria kongamano hilo la utatuzi wa masuala ya mirathi, uchumi na malezi lililoandaliwa na mkuu wa Dar es salaam Paul Makonda.
Hivyo makala KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA
yaani makala yote KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/kero-za-wajane-dar-kumalizwa-ndani-ya.html
0 Response to "KERO ZA WAJANE DAR KUMALIZWA NDANI YA MIEZI MITATU -RC MAKONDA"
Post a Comment