title : KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA
kiungo : KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA
KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA
Na Woinde Shizza, Michuzi TV Kilimanjaro.
KATIBU Tawala wa Mkoa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour amewataka wafanyabiashara kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuitumia Bandari ya Tanga katika kusafirisha mizigo yao kwani hivi sasa imeboreshwa kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza katika kikao kati yake na waandishi wa waandishi wa habari wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo amesema wafanyabiashara wengi kutoka mikoa hiyo wamekuwa wakitumia kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na changamoto ambazo zilikuwepo hapo nyuma lakini kwa sasa Bandari ya Tanga imeboreshwa.
Ametumia nafasi hiyo kuipongeza Mamalaka ya Bandari ya Tanzania chini ya uongozi wa Mhandishi Deusdedit Kakoko kwa jitihada kubwa za kuboresha miundombinu na utoaji wa huduma katika kiwango cha hali ya juu katika bandari ya Tanga na kuwa mkakati huo utaifanya bandari hiyo kuwa kimbilio la wafanyabiashara na wawekezaji. "Tunawaomba wafanyabiashara watumie hii Bandari ya Tanga kwani sasa hivi imeboreshwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mitambo mikubwa ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kurahisisha utoaji huduma,"amesema Mhandishi Aisha.
Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Tanga, Percival Salama amesema kuwa bandari hiyo imeweza kuhudumia tani 506,000 Kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 ambapo hadi kufika Juni mwaka huu watakuwa wamehudumia tani 700,000.Amesema bandari hiyo ina jumla ya mitambo 42 kwa sasa, ambapo kwa mwaka 2018/2019 imeagiza mitambo 20 kati ya hiyo mitambo 16 imeshawasili sawa na asilimia 80 .
Ameongeza hivi sasa changamoto ya suala la mitambo katika bandari hiyo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu, hivyo kuwataka wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro kujitokeza Kwa wingi kuitumia bandari hiyo.
"Bandari ya Tanga ya sasa hivi si ile tuliyoizoea zamani, sasa hivi bandari imeboreshwa sana ikiwa ni jitihada za Mkurugenzi Mkuu wa bandari Tanzania, Mhandisi Deusdedit Kakoko lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wote waliokuwa wakitumia bandari zingine wanarudi nyumbani kwani sasa kumenoga,"amesema Salama.
Amefafanua bandari ya Tanga ndio bandari pekee Afrika yenye uwezo wa kuhudumia nchi saba kwa kutumia mpaka mmoja, ambapo nchi hizo ni Malawi, Zambia, DRC Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.
Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro muhandisi Aisha Amour akiongea na waandishi Wa habari katika mkutano Wa waandishi Wa habari ulioandaliwa na mamlaka ya bandari ya Tanga uliofanyika Leo katika ukumbi Wa mikutano Wa mkuu Wa mkoa Wa Kilimanjaro.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Hivyo makala KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA
yaani makala yote KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/katibu-tawala-atumia-waandishi-wa.html
0 Response to "KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA"
Post a Comment