title : JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO
kiungo : JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO
JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO
Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV
Klabu ya Soka ya Juventus ya Italia imeweka rekodi mpya barani Ulaya na nchini Italia baada yakutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini humo maarufu kama Serie A mara nane mfululizo. Hii inakuwa timu ya kwanza kuweka rekodi hiyo, ambapo hakuna timu katika Ligi tano bora la Ulaya iliyofanya hivyo.
Juventus maarufu kwa jina la Bianconeri ilikuwa ikihitaji alama moja tu katika mchezo wake waliotandikwa bao 2-1 na SPAL, hivyo ikashindikana kutangaza ubingwa huo, katika mchezo wake dhidi ya Fiorentina, Juventus iliondoka na ushindi wa bao 2-1, hivyo kutangaza ubingwa huo.
Katika mchezo huo dhidi ya Fiorentina, Juventus walitoka nyuma kwa bao la Nikola Milenkovic dakika ya 6, kabla ya Alex Sandro kusawazisha dakika ya 37 na bao lakujifunga la Beki wa Kati wa Fiorentina, Germàn Pezzella dakika ya 53, hivyo kufanya jumla ya bao 2-1.
Ushindi huo umepelekea Juventus kutwaa taji la Serie A mara 8 mfululizo, rekodi ambayo haijawekwa na timu yoyote katika bara la Ulaya. Ikiwa na mchezo 150 katika Uwanja wake wa nyumbani, imeshinda michezo 127, mabao yakufunga 335.
MAX ALLEGRI AWEKA REKODI YA KOCHA WA KWANZA KUTWAA MATAJI MATANO MFULULIZO
Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri baada ya timu hiyo kutwaa Ubingwa wake mara nane mfululizo, anakuwa Kocha wa kwanza kutwaa mataji matano ya Ligi (Serie A).
Allegri anatwaa mataji hayo matano baada yakuachiwa mikoba na Kocha Antonio Conte aliyetwaa mataji hayo mara tatu.
Rekodi hiyo inamuweka Kocha huyo katika nafasi ya pili, nyuma ya Giovanni Trapattoni anayeshikilia mataji Saba ya Serie A.
Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri
Hivyo makala JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO
yaani makala yote JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/juventus-yaweka-rekodi-mpya-ulaya-na_20.html
0 Response to "JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO"
Post a Comment