title : DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA
kiungo : DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA
DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA
Na Woinde Shizza Michuzi TV , Arusha
Watanzania wametakiwa kudumisha amani na upendo uliopo katika nchi yetu kwani ndio zawadi pekee tulioachiwa na mwenyezi mungu.
Hayo yamebainishwa na nabii mkuu Wa kanisa la Ngurumo ya upako Dr Geordave Kisambale jijini hapa wakati akiongea na waumini Wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha unabii iliofanyika kosongo jiji hapa.
Alisema kuwa watanzania tunayo amani ambayo tumezawadiwa na mungu ivyo niwajibu Wa kila MTU kuienzi ,kuidumisha pamoja na kuilinda.
"Unajua mungu anatupendelea sana Watanzania ametupa amani ya nchi yetu ,ametufanya tunaishi kwa upendo angalieni nchi zingine wanapigana kila siku ,kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani lakini sisi watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu" alisema Geodave
Aidha aliwataka watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia amani yetu na kuivuruga kwani hii ni zawadi ya pekee tuliopewa na mwenyenzi mungu.
Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea nchi yetu ya Tanzania iendelee kuwa na amani pia aliwakumbusha kuwaeka viongozi wetu Wa kitaifa akiwepo Rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania katika maombi kila siku ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.
Aidha amewataka watanzania kutii Sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza Chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.
Nabii Dr Geodave kisambale akihudumia waumini wake .
Hivyo makala DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA
yaani makala yote DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/drgeodave-kisambale-watanzania.html
0 Response to "DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA"
Post a Comment