title : SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA
kiungo : SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA
SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa Ulaya (EU) inafanya warsha na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadiliana namna ya kuboresha sheria na kanuni mbalimbali kwenye uchimbaji wa madini ya Urani hapa nchini.
Wadau kutoka Wizara ya Madini, Tume ya madini, Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Wizara ya Mali Asili na Utalii na Baraza la Mazingira nchini (NEMC) wote kwa pamoja wanajadiliana namna ya kuboresha sheria na taratibu za uchimbaji wa madini yenye mionzi.
Akizungumza kwenye warsha Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Teknolojia na huduma za Ufundi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Dennis Mwalongo amesema kuwa wadau kwa pamoja wataweza kusaidia kuboresha kanuni za uchimbaji wa madini yenye mionzi kwa lengo la kuondoa muingiliano wa sheria hizo katika sekta ya madini.
“Majadiliano haya yatatuwezesha kutoka na kanuni ambazo zitasaidia kwa namna moja ama nyingine katika kuweka mfumo mzuri utakaowezesha uchimbaji madini yenye mionzi kuwa katika utaratibu mzuri na usio na muingiliano kwenye sekta ya madini na mazingira kwa ujumla” alisema Mwalongo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume ya Madini Nchini Dkt. Abdul Rahaman Mwanga ameeleza kuwa wanatarajia kupata utaratibu na mfumo mzuri wa usimamiaji wa madini yatokanayo na mionzi hapa nchini.
Amesema kuwa Sheria zipo lakini kumekuwa na muingiliano wa sheria ambapo kwa kukaa pamoja wadau watawezesha kuimarisha taratibu za madini na kuwa taratibu hizo ambazo zimeboreshwa zitasaidia katika usalama wa mazingira na afya kwa viumbe mbali mbali vinavyozunguka maeneo ya uchimbaji ya madini ya Urani.
“Tuna imani kuwa taratibu tutaziweka sawa ili kuwezesha uchimbaji wa madini ya Urani hapa nchini na matarajio yetu kuwa madini hayo yatakapoanza kuchimbwa hakutakuwa tena na na muingiliano wowote” alisema Mwanga.
Pia ameeleza kuwa sheria na kanuni hizo na uboreshaji wake utakapokamilika kurekebishwa kutawezesha utaoji bora wa huduma kwa wawekezaji ambao wataamua kuwekeza katika uchimbaji wa madini ya Urani hapa nchini.
Naye mshiriki mwingine kwenye warsha hiyo Dkt. Justin Ngaile amesema mfumo mzuri wa usimamizi wa madini ya Urani utawekwa jambo ambalo litasaidia kurahisisha uwekezaji mkubwa hapa nchini.
Umoja wa Ulaya ndio mdhamini katika warsha hii ambapo kupitia wataalamu wake wanasaidia uboreshaji wa sheria na kanuni mbali mbali za uchimbaji wa madini yenye Mionzi ambazo zimeingiliana na uchimbaji wa madini na masuala yamazingira.
Baadhi ya maeneo hapa nchini yanapopatikana madini ya Urani ni pamoja na Bahi Mkoani Dodoma na Mkuju Mkoani Ruvuma.
Imetolewa na;
Peter G. Ngamilo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania
Namba ya Simu 0755496515
Hivyo makala SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA
yaani makala yote SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/sheriakanuni-za-uchimbaji-salama-wa.html
0 Response to "SHERIA,KANUNI ZA UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI YA URANI ZAANZA KUBORESHWA"
Post a Comment