MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI

MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI
kiungo : MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI

soma pia


MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI


NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

WIMBI la mamba katika ukanda wa mto Ruvu, kata ya Kilangalanga, Kibaha Vijijini mkoani Pwani linadaiwa kuwa wengi hali inayojenga hofu kwa wananchi ambapo hadi sasa watu wawili wameshajeruhiwa na mamba hao. 

Aidha  wanyama waitwao Kiboko wanadaiwa kuvamia baadhi ya mashamba ya watu na kuharibu mazao ikiwemo mpunga. 

Akielezea tukio hilo, diwani wa kata ya Kilangalanga, Mwajuma Denge aliomba idara husika isikie kilio chao kwa kuvuna mamba badala ya kuwatega. 

"Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana mmama mmoja alijeruhiwa mkono na mamba na alifikishwa Tumbi hospital ambako anatakiwa kiasi cha sh. 500,000 hadi sasa ili aweze kufanyiwa operesheni na matibabu zaidi "

"Wiki mbili zilizopita pia mama mwingine amejeruhiwa makalio na alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi na alitibiwa kisha amehamishiwa hospital ya Tumbi anaendelea na matibabu hadi sasa. "alielezea Mwajuma. 

Mwajuma alisema kuwa, viboko nao ni kero nyingine wanaomba idara ya wanyamapori waende wakaangalie namna ya kuwadhibiti kwani hawajui wanapotokea. 

"Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa alichukua hatua na kufanya juhudi binafsi kupeleka watu wa maliasili ambao wanaendelea na jitihada zaidi." 

"Kutokana na mto kujaa na kuweka maji ya rangi ya tope wameshindwa kuwapata mamba hao, na wameacha zoezi hilo, watarudi baada ya wiki moja. "alielezea. 

Nae,  makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,ambae pia ni diwani wa Kikongo Fatma Ngozi alisema tatizo hilo, lipo na kata zilizopita mto huo ikiwa ni sanjali na Dutumi, Mtongani, Kwala,na Kikongo .

Alifafanua, mamba waliwahi kuvunwa tangu miaka ya 90 hivyo wamejaa inabidi wapunguzwe. 


Hivyo makala MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI

yaani makala yote MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/mamba-wageuka-kero-kwa-wananchi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI"

Post a Comment