title : CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019
kiungo : CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019
CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatoa pongezi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Taifa Stars, pamoja na makocha wao wakiongozwa na Ndugu Emmanuel Amunike, kwa ushindi mnono wa magoli 3 dhidi ya Uganda katika mechi iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo ambayo sasa yanamaanisha kuwa Tanzania imefuzu na itashiriki Mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AfCON 2019) huko Misri, Taifa Stars imetutoa Watanzania wote kimasomaso na kumaliza kiu na hamu ya muda mrefu ya wapenzi wa soka, baada ya kusubiri kwa miaka 39 kupata nafasi hii tena baada ya kushiriki mashindano hayo mwaka 1980 huko Nigeria.
Ni matumaini yetu kuwa Wachezaji wa Taifa Stars na makocha wao watazichukulia pongezi hizi pamoja na furaha kubwa isiyo kifani waliyonayo Watanzania kama chachu kubwa ya hamasa itakayowapatia ari na mori wa kushindana na timu za mataifa mengine huko Misri baadae mwaka huu na kurejea na matokeo mazuri yatakayowatangaza na kuwauza wao kimataifa na kuinufaisha nchi yetu Tanzania kwa ujumla.
Hongera Taifa Stars, hongera Watanzania. Kila la heri Taifa Stars AfCON 2019.
Imetolewa leo Jumapili, Machi 24, 2019 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Hivyo makala CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019
yaani makala yote CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/chadema-yaipongeza-taifa-stars-baada-ya.html
0 Response to "CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019"
Post a Comment