title : Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima
kiungo : Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima
Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima
Taasisi za kifedha nchini zimekiwo benki zimeshauriwa kuja na mbinu mbadala wa amana ndogo ndogo kwa ajili ya wakulima na watu wa kipato cha kati na chini ili kuweza kukuza mitaji yao na kupunguza umasikini kwa wananchi wa hasa wa vijijini.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Benki ya Mkombozi, Tawi la Iringa mjini hivi karibuni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema kwamba amana ndogo kwa ajili ya wakulima na wafanyabiashara wa kati inakuza mitaji kwenye benki na kukuza uchumi na ustawi wa jamii nchini.
"Achana na amana kubwa kutoka kwa matajiri ni lazima benki za ndani ya nchini zije na mkakati mathubuti wa kuwa na amana ndogo ndogo ambazo ni endelevu ili kuweza kukuza mitaji yao na kuwainua wananchi masikini kwa kipato," aliongeza Lukuvi
"Nataka kuhakikisha wakulima wa iringa wako wengi sana sasa muanze kufanya mpango wa kuwatembelea na nina uhakika mtarudi na pesa nyingi sana," alifafanua Lukuvi
Aliongeza kwamba kuna tabia ya mabenki ya kuwanya'nywa wadaiwa bila kufuata sheria za nchini na ni baada ya kuwapokesha ovyo ovyo, alisema mnatumia mawakala makanjanja ambao wanatangaza matangazo siku ya Jumapili ambapo mahakama zimefungwa na kuendesha mnada kihuni na kuuza nyumba za masikini.
Lukuvi alisema kwamba ni lazima wafuate sheria za nchini katika kuchukua nyumba za watu masikini kwa kuwashirikisha wizara ya ardhi na msajili ili serikali iweze kujiridhisha kwamba sheria za nchini zilifuatwa.
"Pamoja ya kwamba kuna mikopo chechefu lakini ni lazima mabenki yafuate sheria katika kuchukua dhamana ya wateja wao walioshidwa kulipa mikopo waliyokopa serikali haitakubali kuwapa mali za wanachi bila kufuata sheria maana kuna sheria ya jinsi ya kuchukua dhaman za wateja walioshidwa kurejesha mikopo yao kwa wakatim," alisisitiza Waziri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, George Shumbusho alisema kwamba taasisi za kifedha zinapitia katika kipindi chenye changamoto ikiwa pamoja na ukuaji wa kiwango cha mikopo chechefu (growth of non-performing loans).
"Nichukue fursa hii kutanabaisha mbele ya wateja wenu kwamba pamoja na mambo mengine kuporomoka kwa mitaji, kupungua kwa ukwasi ambazo zote kwa pamoja zimeongeza changamoto katika taasisi za kifedha nchini," alisema.
Alifafanua kwamba katika suala la mikopo benki yao kushirikiana na watendaji wa kata na wenyeviti wa serikali za mitaa katika mkoa wa Iringa na maeneo mengine ndani ya nchini.
Aliongeza kwamba benki hiyo imewaelimisha wananchi umuhimu wa kujumuika kuunda vikundi vya watu watano ambavyo hujumuika katika makundi kumi ambapo ni watu hamsini na kuwa ndio msingi wa dhamana yao.
Shumbusho alisema kwamba pamoja na mano mengine benki hiyo ina riba rafiki inayowezesha mkopaji kujikomboa kiuchumi ndani ya muda husika na lengo endelevu la benki hiyo kuwafikia wananchi wa kawaida wengi zaidi na tawi hilo ni la tisa.
Hivyo makala Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima
yaani makala yote Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/benki-zashauriwa-kuja-na-amana-ndogo.html
0 Response to "Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima"
Post a Comment