title : MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation
kiungo : MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya imetoa msaada wa pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni tatu kwa Karapina Foundation ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika harakati za udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na utoaji wa elimu yatonayo na matumizi ya dawa hizo.
Akizungumza leo Machi 29, 2019 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Karama Foundation , Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogars Siyanga amesema mamlaka hiyo imekuwa ikishirikiana na na mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi mbalimbali vya kijamii katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Amesema mamlaka hiyo inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na mashirika hayo huku akifafanua Karapina Foundation ni shirika ambalo linafanya kazi za udhibiti wa dawa za kulevya kwa kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, kutembelea vituo vya kuwasaidia waathirika na dawa na kutembelea vijiwe vyao na kuwashauri waende kwenye vituo vya matibabu.
"Katika kufanya kazi hizo Karama Foundation kupitia Karama Masoud ambaye ndio mwenye kufanya harakati hizo amekuwa na tatizo kutoweza kuwafikia walengwa wengi na kwa wakati, hii ni kutokana na kutokuwa na usafiri .Mamlaka imeamua kumkabidhi pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni tatu ili imsadie katika kazi hiyo.
"Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawataka Karapina Foundation kuitumia pikipiki hii kwa kazi iliyokusudiwa ili kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya .Aidha Karapina Foundation wanatakiwa kuitunza ili pikipikipi idumu muda mrefu,"amesema Kamishina Jenerali Siyanga.
kuona kwa lengo la kuwezesha kazi za udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na kutoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya na kutembelea vit ufanisi wa shughuli muwezesha katika harakati zake za kupambana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kutoa elimu sema itaendelea kushirikana na taasisi mbalimbali zikiwemo za watu bi binafsi pamoja na makundi ya watu
Amefafanua kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikifuatilia namna ambavyo Karapina Foundation imekuwa ikiifanya kazi hiyo kwa moyo wa uzalendo na hivyo imeona ni vema ikatambua mchango wake kwa kumpa pikipiki na kwamba itaendelea kumsaidia kadri inavyowezekana hasa kwa kutambua kazi ya kupambana na dawa za kulevya ni jukumu la kila mmoja wetu.
Pia amesema mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imekuwa ikishirikiana na makundi na taasisi za watu mbalimbali na hivyo wamekuwa wakisaidia makundi hayo kwa nyakati tofauti."Ni jukumu letu mamlaka kuzisaidia taasisi binafsi na makundi ya watu mbalimbali kwani tunaamini kwa umoja wetu tutafanikiwa kukomesha dawa za kulevya nchini.
"Leo hii tumekabidhi pikipiki hii kama kitendea kazi kwa Karama Foundation na tumekuwa tukifanya hivyo kwa taasisi nyingine pia.Kikubwa tunachoweza kueleza kwa leo, tunatambua kazi nzuri inayofanywa na Karama na hivyo katika kuthibitisha kumtambua tumeona anastahili kuwepa pikipiki.Tumekuwa tukizungumza naye Karama mara nyingi na amekuwa akija ofisini kwetu na kufanya mazungumzo .Tumeona tunakila sababu ya kumsaidia ili atekeleza kile ambachoa amekuwa akikifanya kwa shida na hara,"amesema Kamishina Jenerali Siyanga.
Kwa upande wake Karama Masoud ambaye ndio anayeisimamia Karama Foundation , amesema anashukuru kwa msaada wa kitendea kazi ambacho amekipata na kwamba mamlaka imethibitisha kuwa iko pamoja naye , hivyo ameahidi ataendelea kuifanya kazi hiyo kwa uzalendo mkuwa na wa hali ya juu.
"Harakati za kupambana na dawa za kulevya nimeianza muda mrefu , ilifika mahali nikawa nakata tamaa kwani changamoto ni nyingi ikiwemo ya kifedha na usafiri, hatimaye leo hii Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wameona ninastahili kupata pikipiki ili kurahisisha namna ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
"Kwangu sina cha kuwalipa zaidi ya kutambua , kazi ambayo naifanya inatathiminiwa.Naomba nitumie nafasi hii kueleza wazi, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imesimama kidete kukomesha dawa za kulevya .Kwa mazingira yaliyopo na jitihada za mamlaka nina uhakika Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana,"amesema Masoud.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga (wa kwanza kushoto) akiwa ameshika pikipiki leo jijini Dar es Salaam baada ya kumkabidhi Karama Masoud ambaye amekuwa akishiriki katika udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya na kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa hizo kupitia Karama Foundation.
:Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga (kushoto), akiwa ameshikana mkono na Karama Masoud kutoka Karama Foundation baada ya kumkabidhi pikipiki kwa ajili ya kumsaidia kwenye shughuli zake za kudhibiti dawa za kulevya na kutoa elimu kuhusu athari zitokanazo na matumizi ya dawa hizo.Kamishina Siyanga amekabidhi pikipiki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Karama Masoud kutoka Karama Foundation (kushoto) akiwa ameshikana mkono na Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi baada ya tukio la mamlaka hiyo kukabidhi pikipiki kwa lengo la kumuwezesha Masoud kutekeleza majukumu yake.
Hivyo makala MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation
yaani makala yote MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/mamlaka-ya-kudhibiti-na-kupambana-na.html
0 Response to "MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation"
Post a Comment