title : Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti
kiungo : Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti
Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti

Madaktari kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania-MEWATA- Dkt. Selina Mathias (kushoto) pamoja na Dkt. Deograsia Mkapa (kulia) wakiwaelekeza wananchi waliojitokeza kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji.
Baadhi ya wananchi wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila. Huduma hiyo imetolewa bure na Madaktari wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na Madaktari wa MEWATA.

Mtaalam wa Radiolojia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Roselyne Okkelo (kushoto) akimpatia maelekezo Bi. Tima Kombo kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti.

Dkt. Selina Mathias kutoka MEWATA (kulia) akimpima urefu na uzito Bi. Mage Hasunga mkazi wa Kigamboni.

Mtaalam wa Radiolojia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Fadhili Seleman akitumia mashine ya Utrasound kumpima mteja ili kuthibitisha uvimbe ulioonekana.
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) leo wamehitimisha zoezi la kutoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji na kuhudumia watu zaidi ya 130.
Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema zoezi hilo limefanyika bure kuanzia Februari 02 hadi Februari 03,2019.
‘’Tumetoa huduma hii kwa siku mbili ambapo jana tumewafanyia uchunguzi watu zaidi ya 70 na leo tumewafanyia uchunguzi watu zaidi ya 60, kwa wale ambao wamekutwa na matatizo tumewapangia tarehe ya kurudi kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi zaidi’’. Amefafanua Dkt. Sakafu.
Kwa upande wake Daktari kutoka MEWATA, Dkt. Selina Mathias ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kupata matibabu kwa wakati.
Hivyo makala Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti
yaani makala yote Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/zaidi-ya-watu-130-wanufaika-na.html
0 Response to "Zaidi ya watu 130 wanufaika na uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti"
Post a Comment