title : MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE
kiungo : MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE
MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE
NJOMBE
Mtoto mwenye umri wa miaka 7 anaefahamika kwa jina la Recho Malekela mkazi wa kitongoji cha Lung’angali kijiji cha Matembwe wilayani Njombe ameuawa kwa kuchinjwa koromoe na kutupwa katika msitu uliojirani na nyumbani kwao.
Mtoto huyo wa darasa la pili katika shule ya msingi Matembwe ameuwawa ikiwa siku mbili zimepita tangu kikosi maalumu cha kiinteligensia kiwasiri mkoani Njombe kuongeza nguvu katika kuwasaka watu wanaotekeleza mauaji hayo ya kikatili dhadi ya watoto wadogo ambayo yaliomengi yanahusishwa na visasi pamoja imani za kishirikina.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu mara baada ya kushiriki mazishi ya mtoto Rachel na kutoa rambrambi kwa wafiwa Mbunge wa viti maalumu kupitia CCM Neema Mgaya amewata wananchi kuachana na tabia ya kushambulia watu watuhumiwa wa matukio hayo ya ukatili dhidi ya watoto pindi wanapo wabaini na badala yake wawafikishe katika vyombo vyenye dhamana ya ulinzi ili wahojiwe na kusaidia kubaini mtandao wa wauaji hao.
Mgaya anatoa kauli hiyo ikiwa tayari watu wawili wameuawawa na wananchi wenye hasira kali wilayani Ludewa na Mmoja Wilayani Wanging’ombe baada ya kuhisiwa kujihusisha na matukio ya utekaji hatua ambayo imefanya jeshi la polisi kukosa taarifa kutoka kwa watuhumiwa.
Awali akizungumza katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema serikali imeshitushwa na mauaji yanayoendelea na kwamba tayari kikosi kilichosheheni wataalamu mbalimbali wa upelelezi kilichotumwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Siro kimeanza kazi ya kuwabaini wahusika huku kikiwa tayari na kimewashikiria watu kaadhaa kwa mahojiano.
Msafiri amesema mauaji yanayoendelea yanachafua sura ya amani na kudai kwamba damu ya mtoto Rachel itawatafuta popote walipo wauaji na kuwafikisha katika vyombo vya sheria . Baba mkubwa wa marehemu akizungumza na mwandishi wetu amesema mtoto huyo alitekwa mchana wa february mosi akiwa anatoka shambani jirani na nyumbani kwao baada ya kutumwa na mama mzazi kwenda nyumbani kupika maharage.
Nae Bryson Mlote mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe anaeleza historia ya matukio kama hayo kijijini hapo ambapo anasema inaelezwa miaka ya zamani kulitekelezwa matukio kama hayo na kwamba taarifa za kutekwa zianza kusambaa jioni ya februari mbili ambapo zoezi la kumtafuta lilianza saa kumi na mbili na kufanikiwa kumpata majira ya saa nne usiku katika msitu uliojirani na nyumba yao akiwa amekatwa shingoni na kitu chenye ncha kali.
Hivyo makala MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE
yaani makala yote MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mtoto-mwingine-adaiwa-kuchinjwa-tena.html
0 Response to "MTOTO MWINGINE ADAIWA KUCHINJWA TENA NJOMBE"
Post a Comment