title : WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.
kiungo : WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.
WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe Kassim Majaliwa amewasili leo Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Lengo la ziara yake imeelezwa kuwa ni kuweka msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na kukagua vitalu vya mashamba ili kuliboresha zaidi zao hilo.
Aidha katiaka ziara yake,Waziri Mkuu atatembelea katika Wilaya ya Kigoma Uvinza,Kibondo na Kakonko,sambamba na kuitembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani kibondo na kuzungumza nao.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege kigoma
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma
Waziri mkuu akifurahi pamoja na kikundi cha ngoma cha akina mama
Waziri mkuu Kassimu Majaliwa akiwasalimia wananchi waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa kigoma, baada ya kuwasili kwaajili ya ziara ya kikazi.
Hivyo makala WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.
yaani makala yote WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/waziri-mkuu-awasili-kigoma-kwa-ziara-ya.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE."
Post a Comment