title : WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO
kiungo : WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO
WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO
*Asema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu
*Awataka wananchi kulinda barabara zinazojengwa nchini
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WANANCHI wenye tabia ya kutupa takataka katika mitaro iliyopo pembezoni mwa barabara na kusababisha kuziba na kujaa taka imeonekana kumkera Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa(TAMISEMI)Selemani Jafo kutoa onyo kali.
Jafo ametoa onyo hilo leo Februari 26 ,mwaka 2019 wakati ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo akiwa
katika barabara ya Kijichi Toangoma ameshuhudia baadhi mitaro ya barabara hiyo ikiwa imeanza kujaa taka.
"Serikali inatumia fedha nyingi kutengeneza miundombinu ya barabara ,hivyo lazima wananchi nao waitunze ili iwe salama.Wenye tabia ya kutupa taka waache na hii tabia hatuwezi kuacha iendelee,viongozi wa wilaya hakikisheni usafi wa mitaro unapewa kipaumbele," amesema Waziri Jafo.
Wakati huo huo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lianiva kuanzisha kampeni ya usafi katika maeneo yote ya miundombonu ya barabara ili ibaki salama."Nitoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ukiwemo Mkuu wa wilaya ya Temeke kuanzisha kampeni ya usafi.Nataka mitaro yote iwe
safi,"amefafanua.
Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya DMDP ,Waziri Jafo amesema jumla ya Sh.Bilioni 660 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo na kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ambayo yametokana na kukamilika kwa miradi na maeneo mengine bado inaendelea na ipo hatua mbalimbali za utekelezaji.
Waziri Jafo amepata nafasi ya kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Buza ambacho
kinajengwa kisasa na lengo ni kuondoa adha ambayo wananchi wa Buza na maeneo jirani wamekuwa wakiipata.Amefafanua kuwa ujenzi huo wa kituo cha afya unafanyika chini ya ufadhili wa fedha za miradi ya DMDP na kwamba kabla ya kuanza ujenzi huo ilikuwa ni zahanati lakini kwa namna ambavyo kitakuwa kitakapokamilika kitakuwa kituo cha afya.
"Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli kuna mambo makubwa yanaendelea kufanyika nchini ya kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.Wananchi wa Buza ni mashahidi kupitia ujenzi huu wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi," amesema Waziri Jafo.
Amewahakikishia wananchi wa Buza kuwa baada ya ujenzi kukamilika Serikali itapeleka vifaa tiba vyote ambavyo vinahitajika kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora.Pia amesem Serikali itapeleka Gari mpya ya kubeba wagonjwa( Ambulance).
"Tutaleta Ambulance mpya kabisa kwa ajili ya kituo cha afya Buza,lengo ni kuhakikisha mnakuwa mnakuwa na kila kitu ambacho kinahitajika hapa.Hii yote inatokana na dhamira njema ya Rais wetu ya kupeleka huduma muhimu kwa
wananchi wote," amesema Waziri Jafo.
Waziri Jafo ameendelea kutoa shukrani kwa Benki ya Dunia kutokana na misaada ya fedha ambayo wanaitoa kwa Serikali ya Tanzania na kufafanua kupitia fedha hizo katika Majiji,Manispaa na Halmashauri kote nchini miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa na mingine imekamilika.
"Kuna zaidi ya Sh.Trilioni mbili ambazo zinatumika kuboresha miji yote nchini.Na
kwa Dar es Salaam zimetengwa fedha hizo Sh.Bilioni 660 kuendeleza Jiji na ukweli kuna mabadiliko makubwa hata maeneo ambayo yalikuwa hayapitiki, hivi sasa
yanapitika vizuri," amesisitiza Waziri Jafo.

Hivyo makala WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO
yaani makala yote WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/waziri-jafo-awaonya-wanaotupa-takataka.html
0 Response to "WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO"
Post a Comment