title : WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI
kiungo : WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI
WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI
Na Francis Godwin, Iringa.
IMEELEZWA kuwa shughuli za kibinadamu zikiwemo za kilimo zinazofanywa kando kando ya mto Ruaha mkuu na vyanzo vya maji katika mikoa ya Njombe ,Mbeya na Iringa ambavyo vinaelekeza maji yake katika mto Ruaha mkuu ni chanzo cha mto Ruaha kuendelea kukauka na kusababisha baadhi ya wanyama wanaotegemea maji kuanza kufa.
Akizungumza na wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo ya Ruaha kwa ajili ya kuhamasisha jamii ya kitanzania kujenga utamaduni wa kufanya utalii wa ndani katika hifadhi hiyo ya Ruaha na vivutio vingine vya utalii mikoa ya nyanda za juu kusini , mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ruaha Iringa Izumbe Msindai alisema kuwa mbali ya vifo vya wanyama kuendelea kuongezeka ila magonjwa ya mlipuko kwa wanyama yamekuwa yakiibuka mara kwa mara.
Msindai alisema kuwa hali ya kina cha maji katika mto Ruaha mkuu kimezidi kupungua na kwa sasa maji yaliyopo ni machache sana na hivyo kupelekea baadhi ya wanyama kuanza kufa kwa kukosa maji na wengine kumbumbwana mlipuko kwa magonjwa mbali mbali .
Alisema miaka ya nyuma kipindi kama hiki mto Ruaha mkuu ulikuwa unatiririsha maji kwa kipindi cha mwaka mzima pasipo maji kupunguka ila kwa miaka ya hivi karibuni hadi mwaka huu maji yamekuwa yakikata mapema zaidi na kupelekea wanyama kufa kwa kukosa maji .
" Zimekuwepo jitihada mbali mbali za serikali katika kukabiliana na uharibifu wa vyanzo vya maji vinavyoelekeza maji yake katika mto Ruaha na jitihada hizo zimeendelea kuzaa matunda ila bado jamii inapaswa kuelimishwa zaidi juu ya matumizi sahihi ya maji " alisema
Kwa upande wao kama hifadhi ya Rauha wamepata kutembelea vyanzo mbali mbali vya maji kama kile cha Kimani wilayani Makete mkoani Njombe na kuona maji yakiendelea kutiririka kwa wingi ila sababu ya maji kutofika katika mto Ruaha inawezekana maji hayo yanaishia njiani .
katika hatua nyingine Msindai aliwataka wanahabari nchini kuwa kielelezo chema katika Taifa kwa kuendelea kuhamasisha jamii kuepuka uharibifu wa mazingira pamoja na kuwahamasisha watanzania kutembelea hifadhi hiyo ya Ruaha kujifunza utali wa ndani badala ya kuwaachia wageni kutoka nje .
Alisema kuwekuwa na tofauti kubwa ya gharama za kiingilio katika hifadhi kati ya watalii wa ndani na watalii wa kigeni na kuwa serikali kupitia wizara husika imefanya hivyo ili kila mtanzania kuweza kutembelea hifadhi bila kikwazo chochote na kuwa serikali imeendelea kuboresha miundo mbinu ya kufika hifadhini hapo kirahisi zaidi .
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Iringa Jimson Sanga ambe ni mratibu wa mradi wa kuendeleza utamaduni na utalii nyanda za juu kusini alipongeza jitihada za hifadhi ya Ruaha Iringa kwa kuendelea kutumia mbinu mbali mbali za kuitangaza hifadhi hiyo kwani alisema pamoja na kuwa hifadhi ya Ruaha ni kubwa kuliko zote Afrika ila kwa Tanzania nguvu za utalii zilielekezwa hifadhi za kaskazini ila sasa serikali imepania kuelekeza nguvu zake katika hifadhi za kusini ikiwemo ya Ruaha Iringa .
Sanga alisema iwapo vyombo vya habari vitaendelea na kasi ya kueleza uzuri wa hifadhi za kusini ni wazi Taifa linaweza kuongeza mapato yake kutokana na sekta hiyo ya utalii pekee .
Tembo wa hifadhi ya Ruaha mkoani Iringa wakihangaika kutafuta maji katika vidimbwi kufuatia kukauka kwa mto Ruaha mkuu kutokana na uendeshaji wa shughuli za kibinadamu kando kando ya mto Ruaha kwa mikoa ya Iringa , Mbeya na Njombe (PICHA NA FRANCIS GODWIN).

Baadhi ya wanahabari kutoka mkoa wa Iringa na Morogoro wakiwapiga picha wanyama aina ya Pundamilia waliokuwa wakijipatia malisho yao ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa ,waandishi hao walikuwa katika ziara ya utalii wa ndani kama sehemu ya kuhamasisha watanzania kutembelea hifadhi ya Ruaha Iringa juzi (picha na Francis Godwin)
Hivyo makala WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI
yaani makala yote WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/wanyama-hifadhi-ya-ruaha-wafa-kwa.html
0 Response to "WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI"
Post a Comment