Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti

Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti
kiungo : Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti

soma pia


Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti

Madaktari kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) wakitoa elimu kuhusu uchunguzi wa uvimbe kwenye matiti kabla ya kuanza kwa huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na watalaam wa hospitali hiyo. 
Baadhi ya wananchi wakisubiri huduma ya kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. 
Mtaalam wa Radiolojia Dkt. Ndigwake Mallango akimuelekeza Bw. Diatrick Luoga mkazi wa Kimara namna ya kujifanyia uchuguzi wa awali wa uvimbe kwenye matiti. 
Dkt. Irene Godlove akimsajili Bi. Sadia Sinani kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa awali wa uvimbe kwenye matiti. Huduma hiyo inatolewa bure leo na kesho hospitalini hapo. 


Dar es salaam 

Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) leo imetoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. 

Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema katika zoezi hilo endapo mgonjwa atagundulika kuwa ana uvimbe, sampuli itachukuliwa kwa njia ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

Hivyo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi ili kufanyiwa uchunguzi wa awali ambao unafanyika leo na kesho na huduma hiyo inatolewa bure. 

Akielezea kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti Dkt. Sakafu amesema saratani ya matiti ni namba mbili kati ya saratani zinazowapata wanawake hapa nchini, pia katika vifo vyote vitokanavyo na saratani kwa wanawake Saratani ya matiti ni ya pili. 

“Wengi wanafika hospitalini kwa kuchelewa na ugonjwa unakua umefika hatua ya mwisho na hivyo kusababisha matatibabu yake kuwa na changamoto’’. Amesema Dkt. Sakafu. 

Kwa upande wake Daktari kutoka MEWATA, Dkt. Deograsia Mkapa ametaja visababishi vya ugonjwa wa saratani ya matiti kuwa ni kutonyonyesha, kutofanya mazoezi mara kwa mara na uvutaji wa sigara. 

Dkt. Mkapa amewashauri wanawake endapo wakiona mabadiliko yoyote kwenye mwili hasa kwenye matiti kuwahi hospitalini kwa ajili ya uchunguzi. 

Katika zoezi hilo zaidi ya watu 70 wamefanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji.


Hivyo makala Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti

yaani makala yote Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/wananchi-wajitokeza-kufanyiwa-uchunguzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti"

Post a Comment