title : WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI
kiungo : WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI
WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga amewataka wajumbe wapya wa bodi ya rufani kufanya kazi kwa weledi, kwani serikali imewaamini mpaka kuwapa nafasi hiyo.
Mwakibinga ametoa rai hiyo alipokuwa akizindua rasmi bodi ya tatu ya rufani PSPTB Kwa niaba ya Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (MB) Jijini Dar es Salaam.
“Kuteuliwa hapa ni jukumu kubwa ambalo linakufanya uendelee kujenga kile ulichokuwa nacho siku nyingi hivyo kujenga ni ngumu sana ila kubomoa ni rahisi sana, hivyo nawaombeni sana mmeaminiwa nanyi onesheni uaminifu wenu,hii dhamana mliopewa ni kubwa,msiiangushe serikali” amesema.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa bodi ya psptb Ahmad Kilima amesema katika usimamizi wa maadili ,kanuni za maadili zimeipa bodi mamlaka ya kimahakama kwenye uendeshaji wa mashauri ya kimaadili ,kanuni zimezingatia haki ya msingi kama haki ya kusikilizwa na utetezi wa bodi.
Kilima ametaja kanuni hizo kuwa zimezingatia utaratibu wa haki kwa adhabu za kimaadili ni kubwa zinazojumuisha ,onyo ,kushushwa kiwango cha usajili au kufutiwa usajili kabisa kwa kuzingatia miongozo ya kanuni na tabia ya mtuhumiwa kurudia rudia kosa la kimaadili .
Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga,akizungumza na wajumbe wateule wa bodi ya Rufani ya psptb
Mwenyekiti wa bodi ya Ugavi na Ununuzi wa Umma psptb Ahmad Kilima akitoa Rai kwa wateule hao kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Ununuzi na Ugavi psptb GodFred Mbanyi akitoa neno la Ukaribisho kwa wateule hao
Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga,akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wateule wa bodi ya Rufani ya PSPTB
Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga, Akizungumza na wajumbe hao
Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wateule wa bodi ya rufani
Hivyo makala WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI
yaani makala yote WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/wajumbe-bodi-ya-rufani-psptb-watakiwa.html
0 Response to "WAJUMBE BODI YA RUFANI PSPTB WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA KANUNI"
Post a Comment