TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU.

TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU.
kiungo : TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU.

soma pia


TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wadau mbalimbali hapa nchini kuchukua taadhari kutokana na mifumo ya mvua za wastani na juu wastani zinazotarajiwa kunyeshwa katika maeneo mbalimbali katika kipindi cha cha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi, amesema kuwa baadhi ya maeneo ya nyanda za juu Kaskazini -Mashariki yanatarajia kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Amesema kuwa katika msimu wa mvua za masika ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini-masharika, pwani ya Kaskazini na visiwa vya Ugunja na Pemba, ukanda wa ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa pwani.

"Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi februari mwaka huu katika mkoa wa Kagera na kusambaa katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu pamoja na Shinyanga" amesema Dkt. Kijazi.

Hata hivyo ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa kunyesha katika maeneo ya ukanda pamoja na kuwa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mapema na kuisha mapema.

Ameeleza  kuwa kaskazini mwa mikao ya Kigoma na Morogoro kutakuwa na upungufu wa mvua katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu.

Katika hatua nyengine Dkt. Kijazi amesema kuwa maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani hususani nyanda za juu Kaskazini-mashariki  mikoa ya Arusha na Kilimanjaro yanatakiwa kuzalisha mazoa ambayo yanastahimili unyevunyevu.

Amesema kuwa sekta ya uvuvi katika maeneo ya Arusha na Kilimanjaro inaweza kuathiriwa kutokana na wingi wa mtiririko wa maji katika mabwawa ya samaki, hivyo wafugaji wanapaswa kuimarisha miundombinu ya ufugaji wa samaki.

"Kutokana na mvua za kutosha katika maeneo mengi na kuweza kusababisha uharibifu wa makazi, miundombinu na upotevu wa mali, manejimenti za maafa , watoa huduma za dharura wanatakiwa kuweka mipango stahiki ya kuhakikisha utayari wa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

Akifafanua hali ya kunyesha kwa mvua hizo Dkt.Kijazi amesema kuwa kwa maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria kwa Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita,Simiyu na Shinyanga Dkt. Kijazi amesema kuwa mvua kwa maeneo hayo zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya nne ya mwezi Februari katika Mkoa wa Kagera na kusambaa katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya pili ya mwezi Machi. 

Na mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi na upungufu wa mvua unatarajiwa katika maeneo machache Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Kibondo.

Amesema kuwa katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini ikihusisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga Pwani, Visiwa vya unguja na Pemba pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro ambapo mvua katika maeneo hayo zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya kwanza ya mwezi Machi katika Mkoa wa Dar es salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba na kusambaa katika Mkoa wa Tanga na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro katika Wiki ya kwanza ya mwezi Machi na mvua hizo zinatarajiwa kuwa hadi juu ya wastani katika maneo mengi na upungufu wa mvua unatarajiwa kutokea katika Mkoa wa Morogoro.



Hivyo makala TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU.

yaani makala yote TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/tma-yatoa-mwelekeo-wa-mvua-kipindi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA KIPINDI MACHI HADI MEI MWAKA HUU."

Post a Comment