title : DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE.
kiungo : DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE.
DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE.
Na.John Luhende
Mwamba wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sarah Msafiri , ameishukuru kamati ya amani ya viongozi wa Dini Wilaya ya Kigamboni, kwa kufanya uchaguzi wa viongozi kwa amani na utulivu ,na kusema kuwa kamati hiyo itasaidia kutatua migogoro inayohusu dini na dini , madhehebu ya dini na migogoro ya kijamii kwa njia ya amani .
DC Msafiri ameyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa tukio la uchaguzi huo, ambao yeye kama mlezi wa kamati hiyo amesema kamati hiyo itakuwa kiungo muhimu kati ya serikali na dini .
“Lengo kubwa la kamati hii ni kuhakikisha tunaimarisha amani ya Wilaya na kuangazia maeneo yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani baina ya Madhehebu ama dini na dini, pia inaweza kuishauri serikali katika mabo mbalimbali , mi niwapongeze kwakumaliza zoezi hili kwa amani bila mivutano ‘’Alisema
Aidha DC Msafiri amesema hivi karibuni Wilayani humo kumekuwa na migogoro baina ya dini na Madhehebu ambapo nivigumu kuitatua kisheria ispokuwa kwa mazungumzo ya ndani kiimani .
“Kuna mambo hayihitaji sheria katika kuya tatua nimambo ya kiimani zaidi kamati hii itakuwa inasaidia katika mambo kama hayo”Alisema.
Kwa upande wao viongozi walichaguliwa wametoa ujumbe kwa jamii na wakisisitiza katika kudumisha amani na kuvumiliana katika mambo wanayo hitilafiana Mwenyekiti wakamati hiyo anatoka katika Dini ya Kiislam, Shekhe Iddi Mtitu ambaye ni shekhe mkuu wa wa Wilaya ya Kigamboni, amesema wanadamu wote ni watoto wa Mama mmoja wanatakiwa kuishi kwa maelewano.
“Wanadamu huwa tuna kosea niMwenyezi Mungu pekee asiye kosea tuna paswa kuvumiliana katika tofauti zetu kwa yale tunayohitilafiana ili tudumishe amani yetu “Alisema .
Naye katibu wa kamati hiyo ambaye anatoka katika Dini ya Kikristo Padre Emmanuel Hakiebangimane ,wa parokia ya Mtakatifu Consolata Kigamboni amewataka wananchi na waumini wa dini zote kuishi kwa umoja ushirikiano ,upendo na uaminifu.
Hivyo makala DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE.
yaani makala yote DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/dc-sarah-msafiri-azindua-kamati-ya.html
0 Response to "DC ,SARAH MSAFIRI AZINDUA KAMATI YA AMANI KIGAMBONI ,AYATAJA MAJUKUMU YAKE."
Post a Comment