Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar

Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar
kiungo : Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar

soma pia


Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na wapendwa wao mwishoni mwa wiki walipata fursa ya  kufurahia pamoja siku ya wapendanao yaani Valentine Day katika hafla maalum inayofahamika kama ‘Mkeka na Mvinyo’.

Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam, ilishuhudiwa wakazi hao wakijitokeza kwa wingi sambamba na wapendwa wao ili kufurahia siku hiyo maalum ambapo pamoja na vinywaji vingine waliweza kufurahia mvinyo wa aina mbalimbali unaozalishwa hapa nchini.

Mbali na burudani nzuri ya muziki laini kutoka msanii Maximilian Rioba maarufu kwa jina la Milian, kivutio kingine kwenye hafla hiyo kilikuwa ni matumizi ya mikeka ambapo baadhi ya washiriki walipata fursa ya kuketi kwenye mikeka iliyoandaliwa sambamba na meza fupi wakipata vinywaji, vyakula huku wakifuatilia burudani ya muziki iliyokuwa inaendelea.

“Hii ni hafla yetu ya kwanza ya Mkeka na Mvinyo kati ya hafla nyingine nyingi za aina hii zitakazo fanyika SikuKuu ya Pasaka, Msimu wa Sabasaba, na mwisho wa mwaka yaani Likizo Time. Tunashukuru kuona hafla hii imepokelewa vizuri na wadau na  tunawaahidi mambo mazuri zaidi yanakuja kupitia Mkeka na Mvinyo waendelee kutuunga mkono,’’ alisema Bi Caroline Kirwanda Mratibu wa hafla hiyo kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR).

Aliwashukuru baadhi ya wadau muhimu katika kufanikisha hafla hiyo kuwa ni pamoja na  kampuni ya uzalishaji wa mvinyo ya Alko Vintages ya jijini Dodoma, Hoteli ya Whitesands, Bodi ya Utalii  Tanzania, (TTB), GS 1, pamoja na kampuni ya magazeti ya TSN wazalishaji wa magazeti ya Daily News pamoja na Habari Leo.

Bi Kirwanda aliongeza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo utakaozinduliwa hivi karibuni unaolenga kutangaza utalii wa ndani pamoja kuvumbua fursa mbalimbali za kibiashara ndani ya nchini kwa lengo la kukuza uchumi unaofahamika kwa jina la ‘Domestic Tourism Promotion Initiative’ (DTPI).

“Tunahitaji kuhamasisha zaidi matumizi ya bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wetu kama taifa,’’ aliongeza  bi Kirwanda.

Kwa upande wake, Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Alco Vintages , Sweetbertha Rwabizi alisema ushiriki wao kama wazalishaji wa  mvinyo wa ndani  kwenye hafla hiyo unalenga kuhamasisha zaidi matumizi ya bidhaa hizo kwa kuwa tofauti na kuuza bidhaa zao pia walipata fursa ya kukutana moja kwa moja na watumiaji wa bidhaa hizo na hivyo kupata mrejesho kutoka kwao huku pia wakijenga uelewa zaidi kwa watumiaji kuhusu vinywaji hivyo.

“Iwapo watanzania watabadirika na kuanza kutumia bidhaa hii ya mvinyo unaozalishwa hapa nchini, inaweza kukuza soko la wakulima kwa zaidi ya asilimia 80 kutokana na bidhaa hii kuzidi kupata watumiaji kadiri siku zinavyokwenda.’’ Alisema.
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya uzalishaji wa mvinyo ya Alko Vintages ya jijini Dodoma, Sweetbertha Rwabizi (kulia) akimuhudia mmoja wa  wageni waliojitokeza kufurahia pamoja siku ya wapendanao yaani Valentine Day katika hafla maalum inayofahamika kama ‘Mkeka na Mvinyo’ iliyofanyika katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja na agenda nyingine hafla hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya mvinyo unaozalishwa hapa nchini.


Hivyo makala Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar

yaani makala yote Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/tamasha-la-mkeka-na-mvinyo-lafana-dar.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar"

Post a Comment