SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA

SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA
kiungo : SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA

soma pia


SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA

Jengo la Vyumba vya Madarasa (4) ya Shule ya Msingi Karama, Vimejengwa na World Vision Rukoma AP, vikisubiriwa kukabidhiwa, World Vision tayari wamejenga na Kukabidhi vyumba (2) Shule ya Msingi Luzila Katani Rukoma.
Vifaa vilivyokusanywa kwa Nguvu za Wananchi Kata Rukoma, vikiwa tayari eneo La Ujenzi wa Sekondari ya Kata (Abutaraka), kinachosubiriwa ni Serikali kutenga kiasi kilichopendekezwa ili shughuli ya Ujenzi iendelee 
Wanafunzi wa Darasa la pili Shule ya Msingi Luzila wakiendeea na masomo kama walivokutwa na kamera yetu, Hali kama hiyo inawakumba pia Darasa la sita, changamoto kubwa ni wakati wa mvua, na kuandika, tayari Rasimu ya Bajeti imependekeza Kiasi cha Shilingi Milioni 40 kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa yote mawili ingawa uhitaji ni madarasa saba.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba Vijijini Ndg. Evalista Babyegeya akisaidiwa na Mwenyekiti wa Vijana Ndg. Philipina, katika zoezi la Upandaji miti, ambapo CCM Kata Rukoma kinatarajia kupanda miti Elfu Tano. 
Mh. Murshidi Ngeze Diwani wa Kata Rukoma, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM Kata Rukoma katika sherehe za Miaka 42 ya Chama hicho katika Kata yao. 
Bibi Husina Sadara mmoja kati ya wazee 200 Ndani ya Kata Rukoma, waliopatiwa Vitambulisho vya Wazee awamu ya kwanza tayari kwa Utekelezwaji wa Sera ya Afya ya kuwapatia Wazee wanaostahili Matibabu bure. 
Ndg. Evalista Babyegeya M/kiti wa CCM Bukoba Vijijini akihutubia Wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa Chama hicho katika Kata ya Rukoma, zilizofanyika Kijiji Nsheshe Januari Mosi, 2019. (Picha zote na Abdullatif Yunus) 

………………….. 

Na. Abdullatif Yunus – Kagera 

Kufuatia Hali ya Elimu katika Kata ya Rukoma , Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imepanga kuboresha sekta ya Elimu katika Kata hiyo kwa kutenga zaidi ya Milioni 500, za kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo, zikiwemo upungufu wa Walimu, Madarasa, Vitabu katika Baadhi ya Shule za msingi na Kubwa ikiwa ni Ukosefu wa shule ya Sekondari katika kata Hiyo. 

Kutengwa kwa Kiasi hicho kwa Kata hiyo kimezzua mjadala mkubwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, cha kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti ya mwaka fedha ujao 2019 – 2020 kilichomalizika hivi karibuni, Msuguano mkubwa ukiwa ni kwanini kiasi cha Shilingi Milioni 260 zimeelekezwa kujenga Sekondari katika Kata hiyo, wakati. Hata hivyo baada ya mvutano huo, hatimae kwa pamoja Baraza hilo limekubaliana kwa pamoja kuhusu Kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 kuelekezwa Kata ya Rukoma ili kundeleza na kuibua miradi mbalimbali ya Jamii na maendeleo kwa ujumla ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya madarasa, Zahanati, Nyumba ya Mwalimu , na Ujenzi wa Shule ya Sekondari. 

Hali halisi kwa sasa inaonesha upungufu wa madarasa kadhaa katika baadhi ya shule Katani humo, walimu, Madawati, Vitabu, n.k hivyo kuna uhitaji mkubwa, na nguvu ya ziada inatakiwa ili kuendelea kuboresha Mazingira ya Elimu katika Kata hiyo, kwani ukiachilia mbali Nguvu za Mashirika wahisani kama World Vision Rukoma AP, ambao wametekeleza miradi mbalimbali kama Ujenzi wa Vyumba (2) vya Madarasa ya shule za msingi Luzila na Kamkole, Choo cha Shule ya Msingi Nsheshe, Kuweka Sakafu Darasa Moja S/M Bituntu, na Uanzishwaji wa madarasa ya kila jumapili kwa watoto wenye mahitaji maalumu, kuna haja kubwa ya Serikali kuweka jitihada kuinua Elimu Kata Rukoma. 

Akitoa salaamu zake katika Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata, zilizofanyika katika kitongoji cha Karama Kijiji Nsheshe, Diwani wa Kata hiyo Mh. Murshidi Ngeze amebainisha Kero kubwa mbili katika kata hiyo, moja ikiwa ni Ukosefu wa Sekondari ya Kata, kwani wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali wa takribani Kilometa 13, kwenda Kata ya Jirani ya Rubale kufuata Elimu hivyo kwa mazingira ya Kijijini na watoto wa kike ni hatarishi sana, na akiongeza kuwa Kata hiyo kwa matokeo ya Darasa la saba Mwaka jana Idadi ya Ufaulu imeongezeka. 

Aidha Mh. Ngeze amebainisha changamoto ya pili kubwa kuwa ni ukosefu wa Umeme katika kata hiyo toka Uhuru, hivyo suala hilo limekuwa likizorotesha maendeleo hata ya Elimu kwani, wamekuwa wakiletwa walimu na kuondoka kutokana na mazingira yalivyo. Tayari katika hali ya Uhitaji wa Shule ya Sekondari katika kata yao, Wananchi wamekwisha tenga Eneo na kusanya vifaa vya kuanzia Ujenzi huo, ikiwemo Mchanga , kokoto ,mawe, na tofali kadhaa, kinachosubiriwa ni Kuanza Ujenzi huo. 

Sherehe hizo za Mazazi ya Chama cha Mapinduzi Kata Rukoma, zimeambatana na Zoezi la Upandaji Miti 5,000 likiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bukoba Vijijini, Ndg. Evalista Babyegeya, kuwapokea wenyeviti wa Vitongoji (3), na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji Bituntu Ndg. Swahibu Sambamba na ugawaji wa Vitambulisho 200 vya Wazee ikiwa ni kutekeleza Sera ya Afya ya kuwapatia Wazee matibabu bure, zimehudhuliwa na Wananchi na wakereketwa wa Chama katika Kata hiyo na Kata za jirani, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama Ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji.


Hivyo makala SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA

yaani makala yote SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/serikali-kupeleka-zaidi-ya-milioni-500.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA"

Post a Comment