PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA.

PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA.
kiungo : PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA.

soma pia


PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA.


















Mtawa
Papa Francis 
Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumikisha kingono watawa wa kanisa hilo na kwamba tatizo hilo limekuwa likiendelea.

Papa Francis alikitaja kisa hicho wakati akilijibu swali kuhusu unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mapadre dhidi ya watawa wakati wa kikao cha waandishi wa habari hapo jana aliporejea nyumbani kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Ilikuwa ni mara ya kwanza ya kwa Papa Francis kukiri hadharani kuhusu tatizo la mapadre na maaskofu kuwanyanyasa kingono watawa.

 Alisisitiza kuwa kanisa katoliki limekuwa likilishughulikia saala hilo kwa muda sasa na akaapa kuchukua hatua zaidi.

Alisema kuwa mtangulizi wake Papa Benedict, alilazimika kufunga shirika la zima la watawa ambao walikuwa wakidhulumiwa kingono na makasisi.

Inaaminiwa kuwa hii ni mara ya kwanza Papa Francis amekiri hadharani kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya watawa wa kanisa hilo kubwa zaidi duniani.

Amesema kuwa kanisa limejaribu kukabiliana na tatizo hilo na kwamba juhudi hizo bado ''zinaendelea''.

Alikiri kuwa makasisi na maaskofu wamekuwa wakiwanyanyasa watawa, na kwamba kanisa "linashughulikia suala hilo".

"Ni mpango ambao tumekuwa tukiendeleza,"alisema.

Hata hivyo Kanisa Katoliki leo limeyafafanua matamashi ya Kiongozi wa kanisa hilo Papa Francis kuhusu kisa cha kile alichokiita kuwa ni "utumwa wa ngono" katika shirika moja la watawa la kifaransa, likisema kuwa alimaanisha matumizi mabaya ya madaraka ambayo yalionekana katika matukio ya unyanyasaji wa kingono.

Mwezi Novemba mwaka jana kongamano la kimataifa la watawa wa kanisa katoliki duniani lililaani "utamaduni wa ukimya na usiri" ambao unawazuia kuzungumzia changamoto wanazopitia.

Siku chache zilizopita jarida la wanawake wa Vatican linalofahamika kama Women Church World lililaani vikali unyanyasaji huo ikiongeza kuwa katika visa vingine watawa wanalazimishwa kuavya mimba ya makasisi hao kwasababu kuwa na watoto-ni kitu kinachoenda tofauti na maadili ya ukatoliki.

Jarida hilo limesema vugu vugu la #MeToo limewasaidia wanawake wengi kujitokeza na kusimulia visa vyao.


Chanzo -DW Swahili & BBC Swahili


Hivyo makala PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA.

yaani makala yote PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/papa-francis-akiri-maaskofu-mapadre.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "PAPA FRANCIS AKIRI MAASKOFU, MAPADRE KUWANYANYA KINGONO WATAWA."

Post a Comment