UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM

UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM
kiungo : UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM

soma pia


UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

OMBI la Shishy Baby kwa JPM si mchezo !

Msanii maarufu nchini kwenye tasnia ya uigizaji wa filamu za kibongo nchini pamoja na kuomba nyimbo za Bongo Fleva Zuwena Mohammed a.k.a Shishy Baby ametoa ombi maalumu kwa Rais Dk.John Magufuli.

Shishy a.k.a Shilole hakuwa na muda wa kujivunga yaani baada ya kupata nafasi tu ya kuambiwa anamwambia nini Rais John Magufuli , basi yeye akasema lake kwa Rais ni moja tu nalo ni kwamba anaomba reli ya kisasa inayotumia umeme itakapokamilika basi yeye amruhusu awe anauza chakula tu kwani hiyo itamtosha kuliko akipewa fedha.

Unajua kayasema wapi hayo?Shishy amesema hayo leo Februari 7 mwaka 2019 ndani ya treni wakati anazungumzia safari ya kwenda kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambayo inajengwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli.

"Kwanza nimefurahi kuwepo hapa na kwenda kuangalia namna ujenzi wa reli hiyo ya kisasa unavyoendelea.Ni muhimu kwenda kuangalia ujenzi huu ambao Rais wetu anasema ujenzi wake unatokana na fedha zetu watanzania kupitia kodi, na mimi kwenye kazi zangu nakatwa kodi,"amesema Shishy Baby.

Ameongeza anaamini reli hiyo itakapokamilika utasaidia kujenga uchumi wa nchi yetu kwani watanzania watakuwa na fursa ya kusafiri kati ya eneo moja na jingine kwa haraka."Hivyo hata kwa wanaofanya biashara watakuwa na uwezo wa kusafiri kwa haraka na mambo yakaenda.Itakapokamilika reli hii tutakuwa tumepiga hatua na tuna kila sababu ya kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ya kuleta maendeleo."

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya wasanii ambao wanaitwa na viongozi lakini wanashindwa kufika, Shishy Baby amejibu ni vema wasanii wanapoitwa na viongozi wao wakafika kwani ni sehemu ya kuonesha nidhamu na heshima na kujichanganya na wengine kuna faida nyingi ikiwemo ya kupata mawazo tofauti na kukutana na watu tofauti.

"Unapoitwa na kiongozi halafu ukakataa kwenda huo ni utovu wa nidhamu.Tunashuhudia wasanii maarufu katika nchi mbalimbali duniani wanapoitwa na viongozi wao wanakwenda na wanazungumza bila tatizo.Hivyo wasanii tunapoitwa na viongozi ni vema tukaenda kusikiliza,"amesema.

Kuhusu treni hiyo amesema , kubwa ambalo kwake linamfurahisha ni kwamba inapita Igunga mkoani Tabora , hivyo matarajio yake itakapokamilika atafanya biashara ambapo akatumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa rais kuwa ,anatamani kufanya biashara ndani ya treni ya kisaa."Rais wangu Magufuli naomba jambo moja tu kwako, hii reli ikamilika na treni ikaanza kufanya safari basi uniruhusu niwe nafanya biashara tu.Hii itanitosha sana kuliko kuewa fedha." 

Wakati huo huo Shishy Baby au Shilole amesema kikubwa ambacho kimemfurahisha kwenye safari hiyo ya kwenda kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa, ni kwamba amekutana na wasanii wengi maarufu na wengine hajawahi kuwaona ana kwa ana lakini leo imewezekana.

Kiongozi wa msafara huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo ameelezea umuhimu wa wasanii kushuhudia ujenzi wa SGR na kufafanua Serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania wote.


Hivyo makala UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM

yaani makala yote UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/ujenzi-wa-reli-ya-kisasa-wamkuna-shishy.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM"

Post a Comment