title : OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI
kiungo : OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI
OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani, imemfikisha mahakamani ofisa tawala wilayani humo, John Mwendamaka kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh. milioni mbili ikiwa ni kinyume na kifungu cha 15 (1)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11/2007.
Ofisa huyo anadaiwa kuomba kiasi hicho, kutoka kwa mtoa taarifa ili aweze kumsaidia mdogo wake kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa.
John Mwendamaka ambae alifunguliwa kesi ya jinai namba 22 ya mwaka 2019 ni ofisa tawala katika ofisi ya katibu tawala wa wilaya ya Kisarawe.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kisarawe Devotha Kisoka, mwendesha mashtaka TAKUKURU Naftali Mnzava, aliieleza mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa milioni mbili kwa ajili ya kumsaidia mdogo wa mtoa taarifa kujiunga na mafunzo ya jeshi.
Aidha mshtakiwa, alikana makosa yote mawili na dhamana ilikuwa wazi hivyo alipata dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kesi hiyo itakuja kwa ajili ya hoja za awali march 5 mwaka huu.
Hata hivyo, kamanda wa TAKUKURU mkoani Pwani, Suzana Raymond aliiasa jamii kufuata taratibu, kanuni za sheria za nchi ili kwenda na kasi ya awamu ya tano, chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
Pamoja na hayo ,Suzana alisema kuomba na kupokea rushwa ni kosa kisheria hivyo kila mmoja ajiepushe na vitendo hivyo.
Hivyo makala OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI
yaani makala yote OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/ofisa-tawala-kisarawe-adaiwa-kuomba.html
0 Response to "OFISA TAWALA KISARAWE ADAIWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI MBILI"
Post a Comment