title : NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA
kiungo : NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA
NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe.Stella Ikupa ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu, kuwahamasisha wanachama wao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF )ulioboreshwa ili waweze kupata uhakika wa matibabu.
IKUPA ametoa wito huo wilayani Itilima katika ziara yake wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya, Viongozi wa Vyama vya wenye ulemavu na baadhi ya wenye ulemavu wenyewe wakati wa ziara yake wilayani humo Februari 25, 2019, ambayo ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu nyumba na masuala mbalimbali yahusuyo wenye walemavu.
Amesema ni vema viongozi wa vyama na wenye ulemavu wakapena taarifa na kuhamasishani kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ulioboreshwa, ili wapewe vitambulisho waweze kutibiwa kirahisi.
“Mkijiunga na CHF iliyoboreshwa mkapata kadi mtakuwa na uwezo wa kutibiwa muda wowote, kwa hiyo peaneni hizo taarifa mjiunge watu mnaofahamiana muweze kupewa hivyo vitambulisho mpate kutibiwa kirahisi wakati tukiwa tunasubiri ile bima ya afya kwa kila Mtanzania” alisema Mhe. Ikupa.
Katika hatua nyingine amewaagiza maafisa Ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii kutoa elimu vijijini kwa watu wenye ulemavu kuhusiana na uundwaji wa vikundi na namna ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe. Benson Kilangi akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba amesema katika awamu ya kwanza jumla ya vijana 20 wamepata mafunzo ya utengenezaji wa vitalu nyumba na kufundishwa stadi mbalimbali za kuendesha kilimo biashara na kuongeza mnyororo wa thamani.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Festo Kiswaga amesema miradi ya vitalu katika Mkoa wa Simiyu itatekelezwa kwa viwango na kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akibainisha kuwa vitasaidia kuongeza kipato kwa wananchi katika mkoa na kuwa sehemu ya wananchi kujifunza kilimo bora.
Kwa upande wao viongozi pamoja na watu wenye ulemavu walioshiriki katika ziara hiyo wamemwomba Mhe. Naibu Waziri kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
“Ninaomba Serikali itusaidie tuweze kupata wakalimani wa lugha ya alama ili na sisi walemavu wa kusikia tuweze kupata ujumbe unaokuwa unawasilishwa na viongozi wetu kwenye mikutano na ziara kama hii ya leo hii itatusaidia sana” alisema Mhandi Ntobi Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wasiosikia Mkoa wa Simiyu.
“NaombaWataalam waje watutembelee kwenye vijiji vyetu na kwenye vyama vyetu watusaidie kutupa elimu ya namna ya kuunda vikundi na namna ya kufanya shughuli zinazoweza kutuongezea kipato” Bw. Seni Jitabo mlemavu wa viungo Mkazi wa Zagayu wilayani Itilima.
Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa 27 Februari 2019, akiwa wilayani Itilima Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Lagangabilili na kituo cha maarifa ya jamii Kanadi, ambako amejionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na vijana.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza jambo na Bw. Mhandi Ntobi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu wasiosikia Mkoa wa Simiyu, wakati akiwa katika ziara yake Wilayani Itilima Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( wa pili kulia) alipotembea Ofisi za CCM Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watumishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Mkoani Simiyu(NSSF na PSSSF) mara baada ya kutembelea ofisi za mifuko hiyo wakati wa ziara yake mkoani Simiyu , Februari 25, 2019.
Bw. Seni Jitabo ambaye ni mlemavu wa Viungo akiwasilisha baadhi ya changamoto kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akipokea zawadi ya sabuni kutoka kwa Afisa Vijana wa Wilaya ya Itilima ambaye alimkabidhi kwa niaba ya viongozi wa Wilaya hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
Moja ya Kitalu nyumba(green house) ikatika kata ya Lagangabilili wilayani Itilima, kilichotembelewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa wakati wa ziara yake.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/naibu-waziri-ikupa-atoa-wito-kwa-wenye.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA"
Post a Comment