title : WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5
kiungo : WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5
WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5
NA LUSUNGU HELELA-WMU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameshauri itungwe sheria ya kuhakikisha kila Halmashauri nchini inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira nchini
Hatua hiyo inakuja baada ya agizo la Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati alipokuwa akizindua kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani mwezi Disemba 2018 kuwa kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka.
Amesema hata hivyo tangu agizo hilo lilipotolewa hakuna Halmashauri hata moja iliyoweza kulitekeleza agizo hilo badala yake Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu za uongo.
Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la kulinda Mazingira lililofanyika kitaifa mkoani Tabora, Mhe.Kanyasu ameshauri itungwe sheria itakayowabana Wakurugenzi kutekeleza agizo hilo.
Amesema endapo agizo hilo likapitishwa na bunge na baadaye kuwa sheria Wakurugenzi watalazimika kupanda idadi hiyo ya miti badala ya ilivyo sasa kila Mkurugenzi kutekeleza agizo hilo kama hiyari.
Ameeleza kuwa Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu kubwa za miti iliyopandwa lakini anapokwenda kwa ajili ya kuiona wmiti hiyo imekuwa haionekani na huku wengine wamekuwa wakiibuka na visingizio kwa vile hakuna idadi hiyo ya miti waliyoipanda.
Amesema idadi ya miti ambayo imekuwa ikitajwa na Halmashauri kupandwa imekuwa ya vitabuni isiyo na uhalisia wa aina yoyote.Ameongeza kuwa hata zile Halmashauri ambazo zimekuwa zikijaribu kupanda zimekuwa hazifikishi idadi hiyo hata zikishapanda zimekuwa hazijishughulishi na kufuatia maendeleo ya miti hiyo.
Amesema hali hiyo imepelekea miti iliyo mingi kufa kwa kukosa uangalizi huku mengine kuliwa na mifugo wakati Halmashauri hizo zimekuwa zikibaki na takwimu zile zile za miti waliyoipanda.
Akizungumza Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassani amesema agizo lake lililenga kila Halmashauri ipande miti milioni 1.5 ikiwa ni lazima na sio hiyari kama Halmashauri zinavyotekeleza.
Hata hivyo, Mhe. Samia ameeleza kuwa katika agizo hilo lilikuwa wazi liikitaka kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti ya aina yoyote ile akitolea mfano mizabibu, miti ya matunda ili mradi tu uwe mti bila kujali miti ya aina gani.
Ameongeza kuwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini, Ofisi yake itahakikisha taratibu zinafuatwa za kulifanya agizo hilo liwe sheria.
Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akimwagilia miti mara baada ya kuupanda mara baada ya kumalizika kwa kongamano la mazingira lililofanyika mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kuhusu umuhimu wa kutunga sheria ya kuzibana Halmashauri kupanda miti 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira
Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kongamano la mazingira lililofanyika mkoani Tabora.
Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja wananchi waliohudhuria kongamano la mazingira mkoani Tabora
Miongoni mwa wachangiaji katika kongamano la Mazingira, Juma Elias akitoa mchango wa mawazo wa namna ya kulinda mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na ukataji miti ovyo mkoani Tabora.( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT)
Hivyo makala WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5
yaani makala yote WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/waziri-kanyasu-atoa-mbinu-ya-kuzibana.html
0 Response to "WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5"
Post a Comment