MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO

MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO
kiungo : MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO

soma pia


MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO

*Asema wasipofurahia treni ya umeme,mnataka wafurahie ya dizeli?

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MSANII maarufu nchini Peter Msechu amesema anashangazwa na moyo wa choyo walionao baadhi ya Watanzania ambao kwao ni ngumu kupongeza juhudi za Serikali na badala yake kazi yao ni kutukana wale wanaoamua kutembelea miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Msechu ametoa kauli hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Morogoro akitokea Dar es Salaam kwa usafiri wa treni yeye pamoja na wasanii wengine wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Wasanii wa fani mbalimbali nchini leo Februari 7,2019 wamepata fursa ya kutembelea ujenzi wa reli ya treni ya kisasa ambayo itatumia umeme ambapo Msechu amepongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kwa fedha za ndani.

"Tumefurahi kuwa sehemu ya Watanzania ambao tuliobahatika kuutembelea ujenzi huu wa reli ya kisasa.Ila inasikitisha sana tunapoonekana kwenye miradi mikubwa kama hii ambayo ina tija kwa Taifa letu baadhi ya watu wanatutukana na kusema tumenunuliwa," amesema Msechu.

Ameongeza kuwa ingekuwa leo Makonda angeamua kuwachukua wasanii wa Kenya na Uganda anaamini Watanzania wangelalamika kwanini wamechukuliwa wasanii wa Tanzania hawakuchukuliwa kwenda kuona utekelezaji wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.

"Leo Mkuu wa Mkoa kaamua kutuchukua sisi tuambatane naye msema....mnataka mtuone wapi?Mara ooh mmelipwa sasa sisi kazi yetu nini.Kwani tukilipwa na sisi tukalika kodi Serikalini kuna tatizo gani?

" Mnataka kutuambia huu mradi wa reli ya kisasa hauna manufaa kwa Watanzania wakati kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamika Serikali haiboreshi reli ya kati,leo hii inaboreshwa mnataka tubeze,"amesema Msechu.

Ameongeza msanii huyo kuwa "Serikali hii ni yangu,Rais Magufuli huyu ni wangu ,kodi nalipa kwa fedha yangu,mazuri nitayasema kwa nguvu zangu zote.Niache kufurahia treni ya umeme nifurahie treni ya dizel?Hata mwehu atanicheka."

MSANII maarufu nchini Peter Msechu akiwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda


Hivyo makala MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO

yaani makala yote MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/msanii-peter-msechu-awatolea-uvivu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO"

Post a Comment