Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii

Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii
kiungo : Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii

soma pia


Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii

Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii
  • Zawadi zote zimesogezwa karibu nawe mtandaoni.
  • Faidi vocha ya manunuzi mpaka ya shilingi 50,000.

Miongoni mwa mambo ambayo huufanya mwezi wa Februari kuwa mashuhuri ni uwepo wa sikukuu ya wapendanao au ‘Valentine’s Day.’ Sikukuu hii huadhimishwa kila ifikapo Februari 14 ya kila mwaka ambapo watu huwatumia wapendwa wao kadi na maua yenye jumbe mbalimbali za upendo pamoja na zawadi.
     
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya sikukuu hii kuadhimishwa, tayari maandalizi yamekwishaanza kupitia matangazo tofauti kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Katika kuhakikisha Watanzania wanasherehekea sikukuu hii wakiwa na furaha na tabasamu katika nyuso zao, Jumia imezindua kampeni inayokwenda kwa jina la JUMIA LOVES YOU.’ Kampeni hii ambayo itafikia ukomo Februari 16, imezisogeza zawadi zote kwa ajili ya wapendanao karibu na wateja ili waweze kuzinunua kwa njia ya mtandaoni.    

Hakuna mtu asiyependa zawadi, kwasababu humfanya mpokeaji kujisikia wa umuhimu na thamani katika maisha ya aliyeitoa. Kwa upande wa zawadi Jumia imekuja na orodha ya bidhaa zifuatazo ambazo kwa hakika zitajaza tabasamu katika nyuso za wapendwa wote ‘Valentine’ hii:

Marashi na manukato. Je, utapendezwa kupata kumbato au kutumia muda mwingi na mpendwa wako akiwa na harufu isiyovutia puani mwako? Usijali, sikukuu hii hilo litakoma kwasababu kuna ‘dili za kufa mtu’ kwa upande wa marashi na manukato. Kuna orodha kubwa ya marashi na manukato mbalimbali kwa ajili ya wanawake yanapatikana kwa bei nafuu. Mfanye mpendwa wako anukie ili uwe huru kuwa karibu naye muda wowote.    
Vito vya thamani. Boresha mwonekano wa mpendwa wako kwa kumnunulia vito kama vile saa za mkononi, vidani vya shingoni na mkononi pamoja na hereni. Vitu hivi vina mchango mkubwa zaidi katika kumfanya mtu kupendeza na kuvutia au kuonekana wa kisasa zaidi. Bila ya shaka ungependa mpendwa au mpenzi wako kuvutia kila atakapoonekana mbele za watu. Jumia imekuondolea usumbufu ambao unaufikiria ungeupata kwenda kuzunguka kwenye maduka ya sonara. Vito vyote vya thamani unavyovihitaji vimesogezwa karibu nawe kwa njia ya mtandaoni.       
Vinywaji. Bila ya shaka katika kusherehekea sikukuu hii ya ‘Valentine’ utatenga muda maalum wa kupata chakula na mpendwa wako, iwe ni nyumbani au mgahawani. Nogesha mlo au mtoko wako kwa kuagiza kinywaji kupitia Jumia na uletewa mpaka hapo ulipo. Huduma hii ikiwa imetambulishwa hivi karibuni imekurahisishia kupata vinywaji vya aina zote kama vile juisi, bia, mvinyo, wiski, nakadhalika katika sehemu moja. Ingia mtandaoni uperuzi, uchague na uletewe mpaka hapo ulipo. Bila ya shaka utakuwa unafahamu ni kinywaji gani mpendwa wako anakipendelea zaidi.  
Luninga. Yale mambo ya ‘bebi njoo home tu-chill na kucheki movie’ unaweza kuyafanya ‘Valentine’ hii. Kuna luninga za kisasa na mpya kabisa zinapatikana kwa punguzo kubwa la bei pamoja na kupatiwa vocha za bure ya mpaka shilingi 30,000 ili kukurahisishia manunuzi yako. Kwa hiyo, cha kufanya ni kuingia tu mtandaoni, chagua luninga unayoipendelea, weka vocha ya bure ya manunuzi, utashangaa bei itakavyopungua na kisha agiza uletewe mpaka hapo ulipo.   
Simu. Inawezekana umekuwa ukipata tabu kuwasiliana na mpendwa wako kwa njia ya simu kwa muda mrefu. Hali ya kiuchumi, ukizingatia bado watu wanapona majeraha yaliyoachwa na mwezi wa Januari, hivyo basi uwezekano wa kuwa na fedha za kutosha au kutokuwa nazo kabisa ni mkubwa. Usijali, kuna orodha ndefu ya simu mpya, kali na za kisasa zikiwa zimepunguzwa bei pamoja na vocha ya bure ya manunuzi ya mpaka shilingi 40,000! Wahi sasa, ingia mtandaoni na ufanye manunuzi ya simu ili umshangaze mpendwa wako na kumfanya aikumbuke ‘Valentine’ hii mwaka mzima.      
Vyombo vya jikoni. Kwanini usipendezeshe jiko la mpendwa wako msimu huu wa ‘Valentine’? Najua akina mama au dada wanaopenda kupika watakukumbuka sikukuu zote endapo utawashangaza na zawadi ya vyombo vya jikoni. Kuzipata bidhaa zote za aina hii pitia kwenye orodha yenye vyombo vya nyumbani.   

Kampeni ya ‘Jumia Loves You’ itafikia ukomo Februari 16, na siku ya Ijumaa ya kesho kutakuwa na ‘FLASH SALE.’ Kutakuwa na bidhaa zaidi ya 12 zitakazouzwa kwa punguzo zaidi ya 70% kuanzia saa 6 ya usiku wa leo mpaka saa 5.59 ya usiku wa kesho. Miongoni mwa dili ambazo hautakiwi kuzikosa ni ya luninga mpya ya STAR X yenye ukubwa wa inch 32 itakayouzwa kwa shilingi 299,000 punguzo kutoka shilingi 500,000; pamoja na saa ya kisasa aina ya NAVIFORCE itakayouzwa kwa shilingi 55,000 punguzo kutoka shilingi 100,000!   


Ili kupata taarifa zaidi za mara kwa mara, hakikisha hauchezi mbali na tovuti ya Jumia pamoja na kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.


Hivyo makala Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii

yaani makala yote Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/jumia-inakupenda-valentine-hii.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii"

Post a Comment