Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao

Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao
kiungo : Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao

soma pia


Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao

Na Mwandishi maalum

21/02/2019 Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo walioko katika uangalizi maalum (ICU) katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha utolewaji wa matibabu yao.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Idara ya watoto wenye magonjwa ya moyo Dkt. Sulende Kubhoja wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi.

Dkt. Kubhoja alisema chumba hicho chenye vitanda nane kipo katika wodi mpya ya watoto ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati imeanza kutumika mwanzoni mwa wiki hii.

“Mwanzo ilikuwa ni changamoto pale ambapo mtoto alitakiwa kupata huduma ya dharula na kulazwa katika chumba cha uangalizi maalum lakini kuwepo kwa ICU yao kutaharakisha upatikanaji wa huduma hiyo”.

“Kabla ya kuanza kutumika kwa jengo hili watoto walikuwa wanatibiwa katika jengo ambalo watu wazima walikuwa wanatibiwa na hivyo kutokuwa na nafasi ya kutosha. Hivi sasa watoto wana jengo lao ambalo lina nafasi kubwa na kuwafanya wapate nafasi ya kucheza tofauti na ilivyokuwa awali”, alisema Dkt. Kubhoja.

Alisema kutokuwachanganya watoto na watu wazima kutaboresha huduma kwani dawa na vifaa tiba zitakuwa kwa ajili ya watoto na mazingira ya cliniki na wodini yatakuwa rafiki kwao tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi ambaye ni msimamizi wa wodi ya watoto Husna Mzungu alisema kukamilka kwa ukarabati wa jengo hilo ni jambo jema na la furaha kwani kumebadilisha muonekano wa wodi ya watoto ukilinganisha na ilivyokuwa awali.

Husna alisema katika jengo hilo jipya kuna vitanda vya kutosha ambavyo vinasaidia kuwaweka watoto katika mazingira ya nafasi na kuweza kulala mmoja mmoja ukilinganiha na wodi ya zamani ambako kulikuwa na vitanda vichache vya watoto, hivyo kukiwa na wagonjwa wengi walikuwa wanapata tabu.

Jengo hilo lina ofisi nane, vyumba vya madaktari vinne, wodi yenye vitanda 41 kati ya hivyo 23 viko katika wodi ya kawaida, nane chumba cha uangalizi maalum (ICU) na 10 wodi ya kulipia.Gharama za ujenzi na ukarabati wa jengo hilo ni shilling bilioni 1.3 ambapo asilimia 60 ya fedha hizo zimetolewa na Serikali na asilimia 40 zimetolewa na Jumuia ya Kihundu nchini (BAPS Charity).
Wazazi wakiwa katika jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuwapeleka watoto wao kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kupata matibabu.Picha na JKCI 
Picha ya Jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambalo lina ofisi nane, vyumba vya madaktari vinne, wodi yenye vitanda 41 kati ya hivyo 23 viko katika wodi ya kawaida, nane chumba cha uangalizi maalum (ICU) na 10 wodi ya kulipia. Kuwepo kwa jengo hilo kutaboresha huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.


Hivyo makala Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao

yaani makala yote Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/kuwepo-kwa-chumba-cha-watoto-wenye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao"

Post a Comment