Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account
kiungo : Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

soma pia


Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwaonyesha jengo la TAMISEMI (halipo pichani) wakati wa ziara yake na Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na Wakurugenzi kuwaonyesha mfano bora wa matumizi ya Force Account
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwasili katika jengo la TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa kuwaonyesha Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na Wakurugenzi mfano bora wa matumizi ya Force Account.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akielezea namna jengo la TAMISEMI litakavyokuwa wakati wa ziara yake na Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na Wakurugenzi kuwaonyesha mfano bora wa matumizi ya Force Account.

Majid Abdulkarim 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameonyesha matumizi bora ya utekelezaji wa miradi bila kutumia mkandarasi maarufu kama ‘Force Account ‘ kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ,Wenye viti wa Halmashauri, Wakurungezi na Maafisa mipango wa Halmashauri kwa kuwapeleka kwenye mradi wa Ofisi za Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. 

Jafo amefanya ziara hiyo baada ya kikao chake cha maelekezo kwa viongozi hao ambao halmashauri zao zilifaulu vigezo na kusaini fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati awamu ya Pili. 

Akizungumzia Force Account Jafo alisema kuwa nimeamua kutekeleza kwa vitendo yale ninayowaagizaga wakati wote wa maelekezo yangu kuhusu kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yenu. 

Katika ujenzi wa Jengo hili la Ofisi za Wizara tuliamua na kukubaliana kwa pamoja kutumia mfumo ule ule ambao unatumika katika halmashauri zetu sio sisi tunatoa tu maagizo lakin hatutendi na sasa kupitia mradi huu tumeamua kuwa mfano halisi wa yale tunayoyazungumza alisema Jafo. 

Aliongeza kuwa katika mfumo huu wa force Account tumeweza kusimamia jengo hili kupitia kamati nne ambazo ni Kamati ya manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya ujenzi na ile ya usimamizi na ufuatiliaji. 

“Mradi huu umekuwa na tija pia kwa jamii kwani umetengeneza ajira kwa vijana wetu kwani wao ndo wamekua nguvu katika kufanya shughuli zote za ujenzi kuendelea kwa mujibu wa maelekzo ya wahandishi ambao wanatokea Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na msimamizi wa mradi huu”Amesema Jafo 

Wakati huo huo Jafo aliongeza kuwa ujenzi wa Jengo hili la kisasa zaidi linagharimu shilingi billion moja tu Fedha zilizo tolewa na Rais Magufuli kwa kila Wizara kwa ajili ya kujenga Ofisi katika Mji wa Serikali Ihumwa. 

“Nataka niwahakikishie kuwa ujenzi wa jengo hilo umeratibiwa na mimi mwenyewe Waziri wa TAMISEMI ambapo niliwaunganisha viongozi wote wakuu wa Wizara pamoja na watendaji wa Wizara ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka” 

Sasa kama mimi nimeweza wewe kwanini ushindwe na jengo hili limeanza kujengwa mwezi Disemba 2018 na kama mnavyoona sasa hivi jengo limeshafikia hatua ya mtamba wa panya kwahiyo kasi ya ujenzi iko vizuri sana na tutamaliza ujenzi huu ndani ya muda mfupi ujao; Nataka na nyie mkafanye hivi kwenye maeneo yenu alimalizia Jafo. 

Kwa kuongezea Jafo amazitaka halmashauri zilizo pata fedha ya kutekeleza miradi ya Kimkakati kuanza mipango ya utekelezaji wa miradi hiyo mapema iwezekanavyo ili fedha hizo zitakapo wasili katika halmashauri hizo miradi ianze mara moja na ili iweze kumalizika kwa wakati ulopangwa. 

Aidha naye Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Eng.. Zenah Saidi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa fedha hizo na kuhaidi kusimamia kwa umakini na kuhakikisha zinatekeleza miradi huska kwa ufasa na ubora wa miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha hiyo. 

“Ni toe wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa sasa ni wakati wa kutekeleza miradi hii kwa kutumia mfumo wa Force Account kwani kila mmoja wetu kapata kushuhudia kwa macho yake namna ya mfumo huu unavyo tumika na faida zake kazieleza Bi.Zenah 

Kwa kuhitimisha Bi.Zena amewataka viongozi wenzake kuwa makini wakati wa kutafuta wakandarasi wa kutekeleza miradi kwa wengi wao katika makaratasi wanakuwa vizuri lakini katika utekelezaji hakuna kitu. 



Hivyo makala Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

yaani makala yote Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/jafo-aonyesha-mfano-wa-matumizi-bora-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account"

Post a Comment