DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!

DStv yatangaza ofa kabambe ya Family! - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!
kiungo : DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!

soma pia


DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!

Alhamisi Februari 07, 2019. Punde tu baada ya kumaliza ofa mahsusi ya kufunga mwaka iliyokuwa ikifahamika kama ‘’Muda wa kukiwasha na DStv’’ MultiChoice Tanzania leo imetangaza neema kwa wateja wake wapya watakaojiunga na DStv katika msimu huu wa wapendanao ambapo watajipatia zawadi kabambe ya kifurushi cha DStv Family kwa kipindi cha miezi miwili !

Ofa hiyo maalumu ijulikanayo kama ‘Jiunge na Family ya DStv’ ambayo imeanza mwezi huu itaendelea kwa muda wa miezi miwili hadi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu. Katika kipindi hicho wateja wote wapya wa DStv, wataweza kupata vifaa vyote vya DStv kwa shilingi 79,000 tu na kisha kupata ofa ya kifurushi cha DStv Family cha miezi miwili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo katika ofisi za MultiChoice Tanzania, Meneja Masoko Alpha Mria amesema kuwa ofa hii ni muendelezo wa ofa kedekede zinazoletwa na kampuni ya MultiChoice kwa wateja wake mara kwa mara.
Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Bw. Alpha Mria akizungumza na waandishi wakati uzinduzi wa ofa mpya ya “Jiunge na Family Yetu” mapema leo katika makao makuu ya ofisi za MultiChoice Tanzania.

Amesema tofauti na ofa iliyopita ya muda wa kukiwasha na DStv ambapo mteja alikuwa anapatiwa mwezi mmoja wa kifurushi cha DStv Bomba 19,000/- sasa hivi ofa ya kifurushi imeongezwa thamani hivyo mteja mpya sasa anapata ofa ya kifurushi cha DStv Family 39,000/- tena siyo kwa mwezi mmoja tu, bali miezi miwili.

‘’Tunatambua kuwa huu ni mwanzo wa mwaka na majukumu huwa ni mengi hivyo tumeamua kuwatunuku wateja wetu wanaojiunga nasi wakati huu kwa kuwazawadia kifurushi cha Family chenye chaneli zaidi ya 90 kwa miezi miwili” alisema Alpha na kuongeza “Kwa kifurushi hiki, mteja wetu atafurahia maudhui mbalimbali ikiwemo tamthlia maarufu za ndani na nje, michuano ya ligi maarufu za soka duniani kama ligi ya Uingereza, Ligi ya Hispania (La Liga) Ligi ya Italia (Serie A), michezo na burudani nyingine kadha wa kadha kama mieleka, Taikondo, Ndondi, muziki bila kusahau Habari na vipindi vya elimu” huku akifurahia ligi maarufu kama Serie A, La Liga, Ligi kuu ya Uingereza, burudani ya mieleka WWE, ,filamu na tamthilia kali za kitanzania kama HUBA, Kapuni, Rebeca, Kitimtim bila kusahau kipindi maarufu cha umbea maarufu kama Shilawadu Xtra na vingine vingi ndani ya Maisha Magic Bongo DStv channeli (160).

Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Salum Salum amesema ofa hiyo ni kwa wateja wote wapya wanaojiunga na DStv kuanzia leo na kwamba ofa hiyo ni kwa nchi nzima. “Ofa hii ni kwa nchi nzima. Popote mteja alipo anaweza kupata huduma zetu kwani tuna mawakala nchi nzima” amesema Salum.
Mkuu wa kitengo cha mauzo na usambazaji MultiChoice Tanzania Salum Salum akifafanua kwa undani kuhusiana na Ofa mpya ya DStv inayojulikana kama “Jiunge na Family Yetu” mapema leo katika makao makuu ya ofisi za MultiChoice Tanzania.

“Mbali na kuendelea kufungua ofisi katika mikoa mbalimbali, tuna mawakala wakubwa na wadogo kila pembe ya nchi hii. Zaidi ya yote, mtu yeyote anayetaka kuunganishiwa DStv anaweza kutupigia simu maalum 0659 070707 au kutembelea kurasa zetu za Kijamii kama @Dstvtanzania Instagram, @DStv Facebook , @DStv_Tz Twitter na akitujulisha alipo tunamuunganisha na mawakala na mafundi wetu walio katika eneo husika” amesisitiza Salum. Kuhusu wateja waliopo, Salum amebainisha kuwa hivi karibuni MultiChoice itazindua promosheni kubwa na ya aina yake kwa wateja wake hivyo wakae mkao wa kula.
Wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania katika picha ya pamoja mara ya Uzinduzi wa ofa mpya ya “Jiunge na Family yetu” kutoka DStv.


Hivyo makala DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!

yaani makala yote DStv yatangaza ofa kabambe ya Family! Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DStv yatangaza ofa kabambe ya Family! mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/dstv-yatangaza-ofa-kabambe-ya-family.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!"

Post a Comment